ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 21, 2015

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Kilichotokea Jana Wabunge wa Ukawa Kutoka nje na yeye Kutokusimama Wakati Dk Shein Anaingia Bungeni


"Simtambui Dkt. Shein kama Rais wa Zanzibar 
Nataka tu kuweka rekodi sawa. Nilimpinga Dkt. Ali Mohamed Shein hadharani na jana bungeni. Alipoingia Shein bungeni sikusimama kama inavyotakiwa.
Nilikaa chini kupinga uhalali wake. 
Alipoingia Rais John Magufuli nilisimama na kumpa heshima yake kama Rais na kukaa kumsikiliza. Kuendelea kuzomea wakati Rais halali kaingia Bungeni kuzindua Bunge ili wabunge waanze kazi ni kutokuwa na mikakati sahihi. Ilitosha kumzomea Shein na kukaa chini bila kusimama alipoingia kama tulivyofanya. Wenzangu hawakujua pa kuishia. 
Magufuli anapambana na rushwa. Mimi napambana na rushwa. Namwunga mkono katika vita dhidi ya rushwa. 
Anayempinga Magufuli kwa vyovyote vile anatetea wala rushwa na mafisadi. Anayempinga Magufuli ni yule anayeogopa viwanda na mashamba yaliyobinafsishwa kurudishwa Kwa umma".
-Zitto Z Kabwe

4 comments:

Anonymous said...

Kuna kitu kinaitwa uzalendo (Patriotic) nnaimani mueshimiwa zito ni miongoni mwa wazalendo wa kweli. Nchi kwanza maslahi ya chama baadae. Sasa tuseme hawa ukawa wangekuwepo wakati wa kudai uhuru wa Tanzania wangeshauri tukapigane na muengereza ili atupe nchi yetu badala ya njia ya amani aliotumia mwalimu nyerere? Ndio wao si wanapenda vurugu wangependelea vita na muengereza halafu tutizame nani angeumia zaidi? Maana wanachokitamani wao ukawa ni machafuko yatokee Zanzibar. Ni moja ya njia ya kuwashawishi wanzanzibar wasitii sheria na waanzishe mapambano na vyombo vya dola. Na hao ukawa wangetamani machafuko hayo yakeshaanza Zanzibar yatapakae Tanzania nzima yaani hiyo ndio dream yao. Wanashindwa kufahamu yakuwa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar na kabla ya uhuru wa Tanganyika Zanzibar walikuwa na mfumo wa vyama vingi na matatizo yanayoendelea ya uchaguzi hivi sasa Zanzibar ni kama marejeo ya nyakati hizo . Ukawa hawana uweledi wa nini kinachoendelea Zanzibar zaidi ya kupiga kelele na labda yakuwa wana ajenda yao nyengine suala la Zanzibar kama excuse. Lakini kwa vyovyote ninavyoona kwa jinsi ninavyomwangalia Magufuli na vurugu zao za kipuuzi ni sawa na kupoteza muda wao na kuuchimbia kaburi upizani kwani jamaa ni mwanamme wa shoka au kama alivyosema Lowasa kwamba Magufuli ni dume la ngombe sio mchezo. Watanzania wamemkubali na wanaendelea kukumkubali kitendo chochote cha kum'beza katika jitihada zake za kuwaondolea kero zao ni usaliti wa dhahiri juu ya wananchi na kuna kila dalili ya dhambi hiyo ikaja kuwatafuna.
Suala la Zanzibar hakuna mtanzania makini lisie mumiza kichwa. Tulitegemea kwa kuwakutanisha ukawa na power players katika mgogoro wa Zanzibar kama vile dk Mohamed sheni na viongozi wenzie wa CCM pale bungeni ingekuwa moja ya golden opportunity ya kulitafutia ufumbuzi suala la Zanzibar badala yake tulichokiona kutoka kwa upinzani ni utumbo mtupu na kukatisha tamaa kabisa busara haikutumika hata kidogo hovyo kabisa sishangai Dk Magufuli kuwaita watoto tena wa mitaani wanashindwa kufahamu yakuwa magufuli yupo serious kuhakikisha tunasawazisha makosa yetu na kulisogeza taifa mbele kimaendeleo nna hakika kabisa kutokana na kelele za upizani wakati wa kampeni Mr magufuli alitarajia kukutana na watu makini wa upizani bungeni lakini maskini alichokiona yeye pamoja na watanzania ni bure kabisa.

Anonymous said...

ACHA UNAFIKI,UJINGA NA UHUNI.UNAJIFANYA WEWE NI MZALENDO,UNAUJUA UZALENDO WEWE.NI NANI ALIKUPANDISHA DARAJA HILO MPUNGA WA KONDE.WEWE NI MMOJA WA ILE TIMU ILIYOWAIBIA WANANCHI WA TANZANIA USHINDI WAO HALALI WA WAZI BILA KIFICHO KWA KUSHIRIKIANA NA KAILIMA NA KAPILIMBA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI.YAANI MAANDISHI YAKO YAMENICHEFUA SANA,YAMEJAA UHUNI NA USHENZI.KINACHOLETWA NA UKAWA BUNGENI NI KIELELEZO KUWA USHINDI WA KUBADIRI TAKWIMU MEZANI KAMWE SI USHINDI WA WANANCHI WAPIGA KURA.TUMIA MATUSI NA MSAMIATI WOWOTE ULIO NAO KWA MIAKA HII MITANO KABLA YA UCHAGUZI MKUU UJAO WEWE MWIZI UTAIPATA, NASEMA UTAISOMA NAMBA, BUNGENI NA NJE YA BUNGE.WAPIGA KURA WANALIA,KILIO CHAO WAMEIBIWA, WIZI WA KURA,WIZI WA KURA,WIZI WA KURA,WIZI WA KURA.

Anonymous said...

Yani mchangiaji ..anonymous at 11:36

Kabla hata sijasoma maoni yake nilivyoona hiyo miandishi basi nilijuwa ni wale wahuni waliokuwa wakipiga kelele bugeni wakati mueshimiwa raisi Maghufuli anataka kuhutubia bunge. Vurugu na matusi, uwongo,ulaghi,utapeli, ukanda, vitisho. sio sera za kuwashawishi watanzania kuunga mkono chama cha siasa. Sumaye anaskendal za kujibinafshia mashamba ya serikali kwa mabavu kutoka kwa wananchi. Nae Lowasa kaiuzia serikali mitambo feki ya kuzalishia umeme ilio igharimu serikali upotovu wa mabilioni ya pesa na kila anapotakiwa kulitolea ufafanuzi suala hilo jibu lake linakuwa suala hilo ni gumu. Gumu? Nini maanaake? Kachukua hela ya wanyonge kwa manufaa yake binafsi. Sasa huu kama si wizi kitu gani? Sasa wanajaribu kutumia excuse ya uwongo wa kuibiwa kura ili watu walisahau suala la Richmond lakini nnaimani mzee wa kumbu kumbu Mueshimiwa John P Magufuli hajasahau tunamuomba aharakishe mahakama ya mafisadi ili Lowasa aburuzwe mahakamani kwenda kulitolea ufafanuzi suala la Richmond.

Anonymous said...

Kama role model wako ni wabunge dizaini ya akina Lema,Sugu si ajabu hapa ndipo mwisho wa uwezo wako wa kufikiri.Tumekusamehe bure..