Advertisements

Wednesday, November 18, 2015

Kobe 201 wakamatwa uwanja wa ndege wakisafirishwa nje ya nchi na Mabegi


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia jana na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum (sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia. 
Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs). 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni baada wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola. 

(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)
Paparazi blog

2 comments:

Anonymous said...

Kobe pamoja na udogo wao wamekamatwa pale uwanja wa ndege lakini wale Twiga na urefu wao woooote hawakukamatwa kabisaaaa kweli nchi inaongozwa na kitengo!!

Anonymous said...

Hiyo ndio Tanzania yetu. ESCROW watu wamezoa kwa viroba na hakiulizwa mtu! Twiga kama unavyosema mdau wanaingizwa kwa ndege watunwakiona kimya. Mhe. JPM Rais wa awamu hebu yaone haya majanga na uyavalie njuga?!!