
Badala yake, Mkwasa amewaomba radhi Watanzania kwa kipigo hicho kinachofanya jumla ya mabao yote kuwa 9-2 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkwasa alisema kwa miaka 25 aliyofundisha soka, hajawahi kuongoza timu na kufungwa idadi hiyo kubwa ya mabao.
"Matokeo haya yamenihuzunisha kupita maelezo," alisema Mkwasa.
Alisema wachezaji wake walipambana vya kutosha kiasi cha kufika hatua ya mwisho kabisa ya uwezo wao dhidi ya timu bora Afrika.
"Kama ambavyo Mtanzania yeyote ameumizwa na matokeo haya, ndivyo mimi pia. Naomba radhi kwa matokeo haya.
"Hata kama tungefungwa, lakini siyo kwa idadi ile ya mabao, kweli hakuna anayefurahi matokeo kama haya,' alisema Mkwasa.
Alisema kufungwa kwa Stars kunatokana na ubora wa timu waliyocheza nayo. "Wachezaji wao walikuwa bora kila idara kulinganisha na wachezaji wetu.
"Hatuna wachezaji wenye kariba kama ya wapinzani wetu...wenye usumbufu na wanaojua kukaba. Hili ni tatizo kwenye timu yetu.
"Wenzetu wana wachezaji wengi wazoefu na mechi za kimataifa na wote wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi," alisema.
"Pamoja na matokeo haya mabaya, sina mpango wa kujiuzulu kama watu wanavyoshauri. Nitaendelea kuifundisha Stars na nawaomba wananchi waiunge mkono timu."
Stars sasa italazimika kusubiri harakati zingine za kucheza Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
CHANZO: NIPASHE
3 comments:
Mmatumbi at best.Swala la kuwajibika ni ndoto.
Nnasema tena. Kama timu ya taifa tujitoe mashindano ya kimataifa, tujipe lengo la miaka mitano. Tukubliane mikakati ya kuboresha na kubadilika, turudishe Umiseta LABDA na Umishumta, tuanzishe ligi za vilabu B, C, hata na D. Tuendekeze jitihada za Airtel na Coca cola cup, tupeleke walio wasomi na weye vipaji kwenye mafunzo ya ukocha na viungo Cuba, Ujerumani etc. Kubadili mfumo wa Ligi iwe ya kulipwa. Tubqdili mfumo wa mazoezi utakaoendana na lishe na vitamins. Etc. Tufanye haya kwenye soccer na hata riadha muone Mabadiliko na hatimae baada ya miaka 15, mafanikio ya makombe na medali.
Basi tutakufuza kazi maana tunakupa heshima hutaki tumekuweka hapo na tunaweza kukutoa
Post a Comment