Mwaliko wa Misa Takatifu ya Kumwombea Marehemu Nyamiti Ivan Lusinde
1 comment:
Anonymous
said...
Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Ama baada ya kumuombea dua marehemu, nawasihi sana Watanzania wenzangu tuwe na moyo wa huruma kwa wazazi na ndugu wa marehemu. Nasema hivi kwa sababu kuna Audio clip inasambazwa sasa hivi, imerekodiwa na mdada wa Kitanzania kwa watu wa DC mtakuwa mnamfahamu. Kwa kweli kitendo alichofanya dada huyu si cha kiungwana. Hakuwa na sababu ya kueleza hadithi yote kuhusu sababu ya kifo cha marehemu. Mbaya zaidi anatoa personal information kuhusu magonjwa yaliyokuwa yakimsumbua marehemu. Wote tunaoishi huku ughaibuni tunafahamu kabisa kwamba hata ukienda hospitali, Daktari hawezi kukupa habari zozote zinazomuhusu mgonjwa na swali la kwanza atakalokuuliza ni kama wewe ni ndugu au la. Na kama siyo ndugu utaondoka patupu na hatakuambia chochote. Sasa huyu dada aliyerekodi hiyo clip na kuisambaza, yeye ni nani mpaka akapata uthubutu wa kutengeneza hiyo clip na kwa bahati mbaya Watanzania wenzangu tulivyokuwa watu wa kukurupuka watu wanaendelea kuisambaza na inazidi kuenea. Hebu fikiria kama marehemu angekuwa binti yako na ghafla unatumiwa clip kama hiyo, je itakufariji ama itakuongezea machungu. Nawasihi Watanzania wenzangu wote mtakaopata hiyo clip muifute kabisa ili isiendelee kusambaa na tujifunze kuheshimu siri za marehemu. Nina hakika familia ya marehemu ina taarifa kamili kuhusu yaliyojiri na kwa kushirikiana na vyombo vya dola watalifanyia kazi. Kamwe audio clip kama hii haiwezi kutatua tatizo. Cha muhimu ni kuwaombea wafiwa kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema awafariji. Amina.
1 comment:
Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi.
Ama baada ya kumuombea dua marehemu, nawasihi sana Watanzania wenzangu tuwe na moyo wa huruma kwa wazazi na ndugu wa marehemu. Nasema hivi kwa sababu kuna Audio clip inasambazwa sasa hivi, imerekodiwa na mdada wa Kitanzania kwa watu wa DC mtakuwa mnamfahamu. Kwa kweli kitendo alichofanya dada huyu si cha kiungwana. Hakuwa na sababu ya kueleza hadithi yote kuhusu sababu ya kifo cha marehemu. Mbaya zaidi anatoa personal information kuhusu magonjwa yaliyokuwa yakimsumbua marehemu. Wote tunaoishi huku ughaibuni tunafahamu kabisa kwamba hata ukienda hospitali, Daktari hawezi kukupa habari zozote zinazomuhusu mgonjwa na swali la kwanza atakalokuuliza ni kama wewe ni ndugu au la. Na kama siyo ndugu utaondoka patupu na hatakuambia chochote. Sasa huyu dada aliyerekodi hiyo clip na kuisambaza, yeye ni nani mpaka akapata uthubutu wa kutengeneza hiyo clip na kwa bahati mbaya Watanzania wenzangu tulivyokuwa watu wa kukurupuka watu wanaendelea kuisambaza na inazidi kuenea. Hebu fikiria kama marehemu angekuwa binti yako na ghafla unatumiwa clip kama hiyo, je itakufariji ama itakuongezea machungu.
Nawasihi Watanzania wenzangu wote mtakaopata hiyo clip muifute kabisa ili isiendelee kusambaa na tujifunze kuheshimu siri za marehemu.
Nina hakika familia ya marehemu ina taarifa kamili kuhusu yaliyojiri na kwa kushirikiana na vyombo vya dola watalifanyia kazi. Kamwe audio clip kama hii haiwezi kutatua tatizo. Cha muhimu ni kuwaombea wafiwa kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema awafariji. Amina.
Post a Comment