ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 22, 2015

WADAU WAJITOKEZA KUISAIDIA TIMU YA KIKAPU MBEYA

Na EmanuelMadafa,Mbeya 

Wachezaji 22 wa mpira wa kikapu Mkoa wa Mbeya, tayari wamefanikiwa kuondoka mkoani humo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Taifa CUP, yatakayofanyika Mkoani Dodoma November 22 hadi November 30 mwaka huu.

Wachezaji hao walishindwa kusafiri mapema kuelekea mkoani Dodoma

kushiriki mashindano hayo kutokana na kukabiliwa na uhaba wa fedha hali iliyofanya kuwepo na maandalizi hafifu.

Aidha kufanikiwa kwa timu hiyo kunatokana na kujitokeza kwa Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola, Mkoa wa Mbeya pamoja na Kampuni ya Tbl , amboa wamechangia kiasi kidogo cha fedha kilicho fanikisha safari hiyo.

Akizungumzia juu ya kupokea kwa ufadhiri huo Katibu wa chama cha mpira wa kikapu mkoani Mbeya ambaye pia ni mwalimu wa timu hiyo , Yusuf Nyirenda, amesema kuwa wanawashukuru wadau hao kwa kujitokeza kwa kuchangia kiasi hicho cha fedha .

Amesema kampuni ya Coca Cola pekee imechangia kiasi cha shilingi Mil 1.5 ambapo kwa upande wa Tbl wamechangia kiasi cha shilini laki tano hivyo watajitahidi kutumia kaisi hicho kilicho patikana ili kushiriki mashindano hayo.

Amesema, tayari timu imekwisha ondoka Mbeya November 21, ikiwa na wachezaji 22 kati yao wanawake 11 na wanaume 11 lakini mpaka sasa wamefanikiwa kupata shilingi milioni 2 kati ya milioni 4,700,000 zinazohitajika.

“Kiasi cha shiringi milioni 4,700,000 zinahitajika kwa ajiri ya usafiri wa kwenda na kurudi, chakula, malazi na ada ya kushiriki mashindano haya,”alisema.

Amesema kwa dhati kabisa anaipongeza kampuni ya Coca cola kwani ndio kampuni pekee ambayo imekuwa ikijitoa mara kwa mara kusaidia timu hiyo .

Amesema kutokana na mazingira hayo baadhi ya wachezaji watalazimika kujigharamia wenyewe katika eneo la usafiri hivyo, amewaomba wadau na mashabiki wa mpira huo, kuendelea kjitokeza kwa wingi katika kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki mashindano hayo.

Mwisho.

( Imeandaliwa na Mtandao wa www.Jamiimoja.blogspot.com- Mbeya 0759406070)

No comments: