Na Mwandishi wetu Washington
Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).
Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti nchini Marekani wakionyesha mabango yao
Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari.
Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika.
"Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana Ali.
Pichani ni Bango la waandamanaji wa Zadia
Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"
Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema "Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru" Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwnye Umoja wa Mataifa.
Wapenda amani na Demokrasia wakiwa na mabango yao Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maneno kama vile "Mshindi wa uchaguzi atangazwe", "maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe", "bila haki hakuna amani' na mengineyo.
Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai "tunataka matokeo yetu ya uchaguzi.."
Akizungumza na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo alisema "Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono Wazanzibari katika kudai haki yao"
Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar.
Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.
Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Mpenda amani na Demokrasia Lodi Mohamed akiongea na muandishi wa habari Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia Bwana Thuweni akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia Yussra Alkhary akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
5 comments:
Hiyo zadia ni chama cha wapemba tu.naona simuoni hata muunguja mmoja.mna visa kweli toka lini maandamano yakafanywa na watu.sita.
Hao jamaa hawajakusanyika pale kudai maamuzi ya uchaguzi isipokuwa wamekusanyika pale kuvunja muungano wale wote ni wapemba na mahizibu. Wanasema mtoto akililia wembe mpe siku ya kuvunjika muungano wa Tanzania bara na Zanzibar sku inayofuata waunguja tunavunja muungano na pemba.
Eti mchana wanavaa suti, usiku mikanda ya kulipuka! Wasidanganye watu na hao maskini watoto. Forewarned is forearmed!
mbona wako watu wazima 7 na watoto 6, jumla kumi na tatu. majanga kweli.
Now u have seen the impact ya watu sita after the US cease 944 Millions foreign aid kwa Tz. plz dont be bias post this. Thanks
Post a Comment