Basi la Kampuni ya Taqbiir
lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Katoro-Geita, lilipofika kijiji cha Kisonzo,
tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Desemba mosi mwaka huu,
majira ya saa moja na nusu liligonga Tenka la Mafuta upande wa kulia wa dereva
na kung’oa bati lote na kuua baadhi ya watu papo hapo na wengine walifia njiani
wakipelekwa hospitali ya wilaya ya Iramba.
Kamanda wa Jeshi
la Polisi mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka akitoa taarifa ya ajali kwa
waandishi wa habari (hawapo kwenye picha).
Chanzo: Mo Blog
1 comment:
mungu wangu,yarabi tunusuru na majanga
Post a Comment