Pichani KageBriana akiwa na kombe lake la ushindi.
KageBriana amenyakua ushindi wake kwenye mchuano wa kombe la SETLC Jr. OPEN # 3 L6 singles uliojumuisha wasichana wenye umri wa miaka 12 na chini yake(12 and under) uliofanyika kwenye kituo cha tennis cha SE Tennis and Learning Center SE,Washington DC siku ya Jumammosi Desemba 12. Ushindi huo aliunyakua baada ya kuwashinda wapinzani wake wote, ambapo alimshinda mpinzani wake Amira kwa mabao 6-0 na 6-3. Pia alinyakua kombe lake baadaya kumshinda Isabella DeLeo kwa mabao 6-3 na 6-2.
No comments:
Post a Comment