Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akifurahia jambo na Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 3, 2015. Mkutano huo ni wa kwanza baina ya viongizi hao tangu uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar ufutwe na kuzua malalamiko kutoka kwa wadau kote Duniani. Hata hivyo "Mchafuko huo wa hali ya hewa visiwani" unashughulikiwa kwa vikao ambapo hadi sasa inaelezwa kuwa vionozi wakuu kutoka vyama vya CCM na CU kule Zanzibar, akiwemo Mzee Ali Hassan Mwinyi, wamekuwa kwenye vikao vya kutafuta mnasuo wa kisiasa visiwani humo na mmoja wa wajumbe wa vikao hivyo ni Balozi Seif Ali Iddi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
1 comment:
Kwa huyu bwana balozi seif ally iddi kufanya naye vikao kuhusu matokeo ya uchaguzi zanzibar ni kupoteza muda.la msingi na muhimu zaidi ni kumuepuka.huyu bwana amekubuhu kwa uonngo,ulaghai na ujanja-hila.yeye alikua ndiye mwenyekiti wa timu zote za kampeni za ccm visiwani,na chanzo kikubwa cha anguko hili la ccm visiwani ni yeye.kwa kuwa hii ni aibu na fedheha kubwa hawezi,hawezi kukubali kwamba ccm ilianguka vibaya visiwani,haiwezekani.nikwammbie kitu anapong'ang'ania uchaguzi urudiwe zanzibar muulize anajua maana yake 'fika',amekwisha piga hesabu za gharama zake?nani atakubali ujinga huo? Mheshimiwa Magufuli Huyu huyu Anayepigania Kuokoa na Kukuza Pato la Serikali? Kwa Magufuli tunakuomba seif wa ccm zanzibar usije ukarogwa kumsogelea,atakufukuza ofisini kwake,Hawapendi Wanafiki kama seif,anawachukia sana.kwa hili yuko wazi mno mhe MAGUFULI.
Post a Comment