Monday, December 28, 2015

KIPINDUPINDU CHAINGIA KWA KASI BUSEGA

Na Shushu Joel,Busega

UGONJWA tishio wa kipindupindu unazidi kushika kasi kila kukicha katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kusababisha vifo kwa watu wengi umeingia kwa kasi ya aina yake katika wilaya ya Busega Mkoani Simiyu kwa kufanya watu 8 kulazwa na huku wakiwa chini ya uangalizi mkali wa jopo la wataalamu.
Ugonjwa umepiga hodi jana jioni kwa mgonjwa mmoja mkazi wa kata ya Lamadi kuzidiwa na kupelekwa katika hospital ya mkula iliyo chini ya kanisa na hivyo kuweza kufungulia njia kwa wengine kwa sasa wagonjwa wanazidi kuongezeka na huku wala hakuna eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya wagonjwa hao.
Hali inavyoonyesha uenda ugonjwa huo ukaitesa zaidi wilaya hiyo na hii ni kutokana na wakazi wengi wa maeneo hao kutokuwa na vyoo hasa kando mwa Ziwa Victoria maeneo kama Buyolwa ndogo ambako wakazi walio wengi wanajisaidia katika msitu ulio umbali wa mita chache na ziwa ambalo ndio kiungo kikubwa katika eneo hilo kwani maji utumika kwa shughuli zote za viumbe hai zinazohitajika kutumika.
Wakizungumzia juu ya ugonjwa huo wananchi wa busega wanawatupia lawama watumishi wa afya kwa kusema kuwa wao ni sababu ya kuingia na kueneo kwa ugonjwa huo wilaya humo kwa kusema kuwa wanapoenda kukagua maeneo machafu wanashindwa kuchukua maamuzi ya kuwafungia wahusika hao.
Luge Elikana mfanya biashara wa samaki toka katika mwalo wa Buyolwa ulioko kata ya kiloleli anasema kuwa watu zaidi ya 200 ukutana katika mwalo huo asubui kwa ajili ya biashara ya samaki lakini tatizo lililopo hapa ni ukosefu wa vyoo katika majumba ya watu na hata magesti ya eneo hilo.
Aliongeza kuwa kwa upande wa gesti ni hatari sana endapo milipuko hii ikiendelea kwani vyumba nui vidogo na pia hazifai kwa matumizi ya mwanadamu hivyo lawama ni kwa uongozi wa afya.
Akitoa taarifa za uwepo wa ugonjwa huo Mganga Mkuu wa wilaya Hiyo Godfrey Mbagali alisema kuwa ni kweli ugonjwa huu umetufikia Busega lakini tumesha fanya mikakati kabambe ya kuhakikisha ugonjwa huu ausambai kwa wananchi ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi wote.
Aliongeza kuwa mpaka sasa tumepokea wagonjwa 8 tu na wote wameshapata huduma sitahiki na wako katika uangalizi mkali wa wataalamu wa afya lakini tunamshukuru mungu hali zao zinaendelea vizuri.
Aidha Mbagali aliwataka wananchi wote kuweza kuzingatia yale aliyokuwa akiyasema kipindi cha nyuma ambapo aliwaasa wananchi kuchemsha maji ya kunywa,kunawa mikono wanapotoka kujisaidia na kuongeza usafi zaidi majumbani kwani hii itasaidia kutosambaza maambukizi kwa watu wengine.
Alisema kuwa kuanza juzi tumeanza tena kutoa matangazo kwa wananchi wote ndani ya wilaya kuwakumbusha jinsi ya kuzingatia usafi na kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu pia aliwaambia wananchi watambue kuwa ugonjwa huu ni hatari.

No comments: