ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 16, 2015

MELI YA ROYAL ILIYOKUA IKIELEKEA PEMBA IKITOKEA UNGUJA YAWAKA MOTO

Meli ya MV Royal iliyokuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba imewaka moto leo ikiwa majini katika Bahari ya Hindi. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba chanzo cha moto huo ni hitilafu iliyotokea katika injini ya meli hiyo.

Meli ya MV Serengeti iliyokuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja inaendelea na zoezi la uokoaji katika meli hiyo.
Vikosi vya uokoaji vikizima mato uliozuka katika Meli ya MV Royal leo.
Abiria wakiokolewa na MV Serengeti
Moshi ukifuka kutoka chumba cha injini
Abiria wakitolewa katika Meli ya MV Royal na kuwekwa kwenye MV Serengeti.

No comments: