Saturday, December 5, 2015

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam Awaagiza Wakurugenzi Kuwaondoa Ombaomba Waliko Barabara za Jiji


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko katika barabara za jiji, kwani wanachangia uchafu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Sadiki alisema utekelezaji wa kauli ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya Desemba 9 mwaka huu kufanya usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa ombaomba hao, ambao wanachangia kuongeza uchafu.
“Siwezi kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo wanayofanyia shughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na kutupa ovyo,” alisema.
Alisema viongozi ambao wako katika maeneo ambayo ombaomba hao wanarudi, wahakikishe hawarudi mjini kwa sababu imekuwa ni tabia ya omba omba hao wanaporudishwa baada ya muda kurudi tena jijini.
Aidha, aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwaondoa wapigadebe katika vituo vya daladala kwani wamekuwa kero kwa abiria.

4 comments:

Kush said...

Mungu awabariki, its so sad for the kids,God bless them

Anonymous said...

Tatizo la ombax2 na machinga kwenye traffic lights ni majipu mengine yanayo hitaji kutumbuliwa ASAP.

Anonymous said...

Usafi
Kwanza utuonyeshe ofisi yake kama. Safi
Na nyumbani kwake live alilete hapa magufuli si mjinga

Anonymous said...

Uwii wakwe na mawifi mkomege kuhalibu ndoa za watoto wenu wakiendelea kukaa pamoja si mauso yanawashukaga? Mhh