Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu akifungua rasmi Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha
Mwenyekiti wa muda wa Mkutano wa Baraza Ndg. Daniel Machunda ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha akikabidhi madaraka hayo kwa Mstahiki Meya mara baada ya kuchaguliwa kwa kura 33 kati ya kura 34 zilizopigwa.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Juma Iddi ambaye pia ni Katibu wa Mkutano wa Baraza akitoa muongozo wa namna Mkutano huu wa kwanza unavyoendeshwa kwa mujibu wa kanuni,kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda.
Diwani wa Kata ya Sokon I, Mheshimiwa Calist Lazaro Bukhai(Chadema) akikishukuru baada ya kuchaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Arusha.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ,Mhe Calist Lazaro Bukhai akiwa na Naibu Meya wake Viola Lazaro Likindikoki kwenye Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani
Diwani wa Kata ya Kaloleni Mhe Lewis Kessy (Kushoto) na Diwani wa Kata ya Levolosi Mhe. Efatha Nanyaro wakiwa kwenye Kikao cha kwanza cha Baraza la madiwani wa Jiji la Arusha
Mhe. Abdulrasul Tojo (kulia) ambaye ni diwani pekee wa CCM kwenye Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha alipokua akiomba kura katika nafasi ya Naibu Meya wa Jiji hilo.
Mstahiki Meya Mhe. Calist Bukhai (aliyevaa Taji) Naibu Meya Mhe. Viola Likindikoki (tatu kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu (nne kulia), Mkurugenzi wa Jiji, Ndgugu Juma Iddi (tatu kulia) pamoja na Madiwani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Kikao cha Baraza la madiwani.
3 comments:
HONGERA SANA WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA,HONGERA SANA WANANCHI WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA; KWANZA KWA MSIMAMO THABITI ULIOJAA UKWELI NA NIA YA WAZI YA KUYAKUBALI MABADIRIKO.WAKATI WA MABADIRIKO NI SASA,TUTACHELEWA DHAMIRA YETU KWA MIAKA MITANO IJAYO LAKINI,UZALENDO WA KUYAKUBALI NA KUYAENZI MABADIRIKO UMEJIDHIHIRISHA WAZI.UONGOZI MPYA WA UKAWA-CHADEMA KATIKA KUISIMAMIA MANISPAA YA JIJI LA ARUSHA UWE CHACHU,NURU NA MFANO WA KUIGWA TANZANIA NZIMA NA WANANCHI TUWAUNGE MKONO MEYA,NAIBU WAKE NA MADIWANI HAWA WOOOTE KASORO MMOJA[WA CCM].WATIMIZE WAJIBU WAO KWA WELEDI,UAMINIFU,UBUNIFU.WAWE MFANO WA KUIGWA ILI WANANCHI WA MAENEO MENGINE YOTE NCHINI WAJENGWE IMANI NA KUKUBALI KUBADIRIKA.UKAWA NI YA WATANZANIA WOTE,MBARIKIWE.
Mkuu wa wilaya jembe hongera Wana Arusha
Mkuu wa wilaya Jembe Hongera Wana Arusha!!
Post a Comment