Tuesday, December 8, 2015

MNYIKA: RIPOTI ZA MWAKYEMBE KUHUSU MADUDU BANDARINI ZIWEKWE WAZI, SIO KUTUMBUA MAJIPU TU


Baada ya kuwa kimya tangu ashinde Ubunge, Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika ameibukia kwenye sakata la ubadhirifu kwenye Mamlaka ya Bandari nchini na kuitaka serikali kuweka wazi ripoti za Dk. Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta.


Mnyika ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amedai kuwa ripoti za Sitta na Dk. Mwakyembe zimebeba ukweli zaidi kuhusu kinachoendelea bandarini hivyo kuziweka wazi kutasaidia kutibu tatizo lililopo zaidi ya kuwasimamisha watendaji waliotajwa.

Akiyafananisha matatizo ya bandari na majipu anayoyatumbua rais John Magufuli, alisema kuwa dawa yake ni kuyapasua ili kuondoa kiini badala ya kuyatumbua tu.

Dawa ya jipu sio kulitumbua bali ni kulipasua ili kiini cha ndani kitoke, ukikiacha jipu linaanza upya tena linakuwa hatari zaidi, alisema Mnyika.

Kama kweli serikali ya awamu ya tano ina lengo la kufichua ufisadi, basi inapaswa kuweka wazi ripoti mbalimbali za uchunguzi ziwe dira ya kujua kiini cha matatizo kujitokeza katika Mamlaka ya Bandari, aliongeza.

2 comments:

Unknown said...

Ndugu manyika ungekuwa muungwana na watanzania tungekuheshimu kama ungetambua na kupongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na muheshimiwa raisi. Wakati wa kuziwekea vikao ripoti sasa basi ila kinachotakina sasa ni utendaji na ndicho anachokifanya muheshimiwa raisi. Muheshimiwa sio mwanasiasa hana blah blah isipokuwa kazi tu nafikiri unaelewa hilo. Waziri wa taasisi husika ni mtendaji mkuu wa eneo hilo kitu gani kilichowafanya hao waishimiwa mawaziri uliowapendekeza kuwa ripoti zao zifanyiwe kazi kutekeleza maigizo ya hiyo ripoti wakati wao walishakuwa mawaziri na wasimamizi wakuu wa taasisi ilioundiwa hiyo ripoti? Doesn't make any sense. Majipu yataendelea kutumbuliwa chini ya uongozi wa mueshimiwa magufuli na kwa uhakika kabisa huwezi kulipasua jipu bila kulitumbua kwanza na ndicho kinachoendelea kwa sasa na tunaimani kwa muheshimiwa Magufuli ya kwamba chini ya uongozi wake Tanzania iliokuwa gonjwa iliotawalia na majipu kila kona itapata nafuu na kuwa nchi yenye uchumi wenye afya,uwajibikaji wenye afya uliotukuka barani Africa na Dunua kwa ujumla. Na kuwa nchi yenye nidhamu heshima na watendaji makini. Wakati kama huu mueshimiwa raisi akipambana na uozo wa kila aina serikalini tunatakiwa kuwabaini kwa haraka wale wote watakao jaribu kumrejesha raisi asitimize wajibu wake. Watu kama kina manyika kujifanya wanauwezo wa kumkosoa raisi wakati ukweli ni kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha muheshimiwa raisi anashindwa vita vyake zidi ya ubadhirifu na mafisadi. Tumuombee raisi wetu muadilifu mungu ampe nguvu zaidi. Mungu hapendi zuluma kwenye baadhi ya maandiko yake matakatifu mungu ameifananisha zambi ya rushwa na ubadhirifu sawa na mtu kufanya tendo la ndoa na mzee wake. Kwa hivyo tunaimani magufuli atafanikiwa kwa kuwa mungu yupo pamoja nae kwa kuwa napigania haki za wanyonge.

Anonymous said...

Hawana mpya wala nyimbo hawa, baada ya kumpongeza Raisi na aendeleze juhudi zake, unarudisha nyuma, utarudi wewe na wenzako, hapa kazi tu, mbele kwa mbele