Mimi ni mdau wa blog ya Vijimambo na naomba msaada wa hili neno JASUSI maana yake nini. Nakumbuka nilipokua mtoto neno JASUSI lilitumika kama mtu mbya au adui au kwa neno lingine si mtu mwema.
Leo nilipokua mtaani ukazuka ubishi wa maana ya neno hilo JASUSI kila mtu akilitafusili kivyake nikaona ni vyema nililete hapa leo niweze kupata msaada kwa wadau wengine, asante na natanguliza shukurani.
1 comment:
Kwanza kabisa kabla ya kwenda kwenye maana halisi ya jasusi tunapaswa kufahamu kuwa lugha yetu ya kiswahili inamkusanyiko wa maneno mengi ya kigeni kama zilivyo lugha nyingi duniani. Kwa mfano (good) kwa waengereza, wataalam wa lugha wanatuambia asili yake ni ujerumani na neno asilia ni(Gutt).
Kwa hivyo Jasusi ni neno la kiswahili lilotokana na lugha ya kiarabu lenye maana ya mpelelezi au spy na warabu wanalitamka hivyo hivyo kama tunavyolitamka sisi labda tunaweza tukapishana kido katika lafdhi . Na hapana shaka hata sisi waswahili tunalitumia neno jasusi kwa maana ya mpelelezi hasa alietumwa kutoka nchi fulani kwenda nchi nyengine ya kigeni kwa ajili ya kufanya upelelezi.
Post a Comment