ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 16, 2015

OFISI YA RAIS WA AWAAMU YA PILI ALHAJ DKT ALI HASSAN MWINYI

TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI WA KUVAMIWA KWA MAKAAZI YA RAIS MSTAAFU TAREHE 10 DISEMBA 2015

Kuna taarifa zilizosambazwa kupitia kwa gazeti moja la kila siku iliyochapishwa tarehe 15 Disemba 2015 kwamba kuna mtu mmoja alivamia makaazi ya Rais wa Awamu ya Pili Alhaj Dkt Ali Hassan Mwinyi. Aidha, mvamizi huyo aliyejitambulisha kwa majina ya Hafidhi Ali, Mkaazi wa Ilala imeripotiwa katika taarifa hiyo kuwa alifikishwa katika Mahakama ya Kinondoni akikabiliwa na mashtaka hayo ya uvamizi.

Kwa kupitia taarifa hii, natoa taarifa kwamba mtuhumiwa huyo hakukamatwa akiwa amevamia makaazi ya Rais Mstaafu, bali alikamatwa akiwa maeneo jirani na kwa kiongozi wetu huku akijinasibu kuwa yeye ametokea katika makaazi ya Rais Mstaafu. Aidha, Ofisi ya Rais Mstaafu haikuwahi kuwasilisha mashtaka kuhusu kijana huyo. Taarifa hiyo imewashtua wananchi wengi na hivyo kupelekea ufafanuzi huu utolewe.

Imetolewa na
Dkt. Abdullah H. MAKAME
Katibu wa Rais wa Awamu ya Pili
16 Disemba 2015

No comments: