Co-
founder wa Pop Up Bongo Natasha Stambuli akionesha bidhaa za duka lake
la Secret Habit ambalo nalo lilionesha bidhaa zake siku hiyo.
Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali mahiri mjini, Aika Lawere mmiliki wa Mbezi Garden alikuwapo pia
Mbunifu wa mavazi nchini wa lebo ya Branoz Collection, Bahati Kombe (katikati) akipanga bidhaa zake wakati wa Tamasha la Pop Up Bongo lililofanyika juzi Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff.
Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Wauzaji wa bidhaa mbalimbali kutoka duka la Beauty Haven wakiwa kwenye banda lao wakati wa Tamasha la Po Up Bongo lililofanyika juzi Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
Tanya akiwa na wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye Pop Up shop
Atu Mynah akimtaja mshindi wa bahati nasibu siku hiyo
Kutokea banda la Beauty Heaven kulikuwa na bidhaa mbalimbali pia
Natasha akizungumza na mmoja kati ya washiriki waliojitokeza kuonesha bidhaa siku hiyo
Na Mwandishi Wetu
ONESHO la mauzo ya bidhaa mbalimbali
zitengenezwazo na wabunifu wa hapa nchini, Pop Up Bongo lilifanyika hivi
karibuni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Mratibu wa onesho hilo lililofanyikia Triniti Oyster bay,Natasha Stambuli alisema
kuwa zaidi ya wajasiriamali 15 walijiotokeza kuonesha na kuuza bidhaa zao.
Alisema kuwa bidhaa mbalimbali kama vile nguo, vito, viatu na vinginevyo
viliuzwa na wajasiriamali hao walipata wasaha wa kuongeza wigo wao kibiashara
kwa kukutana na wanunuzi.
"Pop Up Bongo inalenga kuwaweka karibu zaidi wajasiriamali na wanunuzi hao
kwa kuwakutanisha mahala hapa na kisha hata wakishafanya mauzo wanakuwa na
wasaha wa kuonana hata baada ya Tamasha hili na kuendeleza uhusiano wa
kibiashara" alisema Natasha.
Pia ametoa wito kwa wanajamii kujenga utamaduni wa kuhudhuria maonesho
mbalimbali ya biashara ili kupanua wigo zaidi wa ufahamu wa aina mbalimbali za
bidhaa ziuzwazo nchini.
Natasha alisema kuwa kwa kutembelea maonesho hayo watapata wasaha wa kufahamu
aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara mbalimbali na kujua ni
wapo pa kwenda kujipatia mahitaji.
Alisema kuwa Pop Up Bongo ikiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
inalenga kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali zitengenezwazo
hapa nchini na wanunuzi kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali wa hapa nchini
kuongeza pia wigo wa biashara zao.
Kwa upande wake Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
alisema kuwa kwa kampuni hiyo inatambua nafasi ya wajasiriamali katika
kuendeleza uchumi wa nchi na ndio maana imeamua kuunga mkono Pop Up Bongo.
"SBL kwa kupitia kinywaji chetu cha Smirnoff tumeamua kudhamini Pop Up
Bongo kwa kuwa ni mahala pazuri kwa wapenzi wa kinywaji hiki kukutana huku
wakijipatia mahitaji yao kadhaa kutoka kwa wauzaji wanaouza bidhaa zao katika
Pop Up Bongo" alisema Shomari.
No comments:
Post a Comment