Rais wa Jamhuri ya
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO)
Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa
wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya
ujenzi wa reli ya kati.
Akitoa taarifa kwa
vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais
Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka
Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinahusika katika utekelezaji
wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard
Gauge"
Amesema pamoja na
kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO
baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia
mchakato wa zabuni hiyo na badala yake imeonekana kutetea kilichofanyika
Aidha Rais Magufuli
amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Benhadard Tito kutoa ushirikiano kwa
vyombo vya serikali vitakavyofanya uchunguzi zaidi kuhusu mchakato wa Zabuni
hiyo.
Pia ameiagiza
Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua
dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika
kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.
Katika hatua
nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Reli
Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na jinsi bodi hiyo ilivyoshughulikia
ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa ya treni.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa
Mawasiliano, IKULU
22 Desemba, 2015

3 comments:
Then waziri WA sheria no Mwakyembe . Sijapata jibu hapa mkuu wa nchi. Mimi naona unatuzuga nakufunika uwozo. Ninachokiona utaishia kumtimua kazi huyo waziri wako. Mengi yataibuka usifikiri watu ni wajinga kihivyo.nina imani kubwa Mwakyembe ana kesi ya kujibu.
Then kusikia na kunukuu mitandaoni yanayosemwa na watu kuhusu watu fulani kuwa wanamakosa bila ya kuwa na taarifa sahihi na tosha za kinteljensia na kujifanya kuwa wewe ni mwerevu ni kujitia ujingani. Being in Tanzania government for a such long time as an outsider of the CCM inner circle i believe magufuli knows who's right and who's not.
Samahani mdau hapo juu. Mimi sikujua kama Magufuli au Mwakyembe ni ndugu zako. Kwani sikuwa najua kama magufuli ana upeo wa hivyo..wa..kuwatofautisha watu wenye dhambi na wasiokuwa na dhambi.kweli kikulacho ki nguoni mwako.
Post a Comment