ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 4, 2015

SIKU YA MTANZANIA SEATTLE, WASHINGTON STATE

Mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini akiwa amewasili uwanja wa ndege wa Seattle tayari kufanya onesho kubwa la vivazi kesho Jumamosi Dec 5, 2015 kwenye siku ya Mtanzania Washington, State.

Ndugu Watanzania wenzangu,

Jumuiya yenu ya Tanzaseattle imekamilisha matayarisho ya kusherehekea Siku ya Mtanzania. Hii ni miongoni mwa Sherehe za mwaka ambazo husherehekewa na Jumuiya.

Njoo ufurahi pamoja na kukutana na wanadiaspora kutoka nchi mbali mbali.

Sherehe hii ni ya kujivunia Utanzania na Uafrika wako kwa kivazi na burudani mbali mbali.

Sherehe hii itaambatana na maonesho ya mavazi ya Kitanzania kutoka kwa Mwanamitindo maarufu Duniani: Asia Idarous Khamsin kutoka Tanzania.

Njoo ujipatie ladha ya Chakula safi cha Kitanzania pamoja na kucheza muziki wa asili ya Kitanzania ukinawirishwa na muziki wa Dansi( Mlimani Paki, Marijani Rajabui n.k bila kusahau nyimbo mwanana za Taarab kutoka visiwa vya Zanzibar)

Jumuiya inakuomba uvae nguo ya Kitamaduni (optional). Pia mutaweza kununua nguo kwenye maonesho ya mavazi siku hiyo hiyo.

Pahala ni:

411 156th Ave NE
Bellevue, Wa 98007


Mlango kuanza kufunguliwa Saa Moja usiku (7pm) - Ratiba kamili itakuwepo siku ya shughuli hii kwa matukio tofauti mbali mbali yakufurahusha.


Kingilio ni Dola 10 kwa mtu. ($10 per person)

Tafadhali mjulishe rafiki na jirani yako.

Karibuni nyote kwa wingi,

Uongozi wa TanzaSeattle, Seattle Washington USA.

No comments: