Monday, December 7, 2015

TAARIFA YA MAANDAMANO UN NEW YORK CITY

Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA) inapenda kuwaarifu Wazanzibari, Watanzania na Wapenda Amani wote ulimwenguni kuhudhuria katika maandamano ya kushinikiza kumaliza mchakato wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika huko nyumbani Zanzibar tarehe 25/10/2015.
Maandamano hayo yatafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/12/2015 kwenye viunga vya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York kuanzia saa nne asubuhi (10:00 AM) hadi saa sita mchana (12:00 PM). Kufika kwenu kwa wingi na kwa wakati ndio mafanikio ya maandamano yetu haya.
Yoyote atakaesikia taarifa hizi anaombwa amuarifu mweziwe.
Asanteni

8 comments:

Anonymous said...

Na nyie mtafikiri kweli mnaeipenda znz wao huko hawajandama nyie kiherehere tu mnatafuta njia ya kupata makaratasi muongopeni mungu

Anonymous said...

Itakua mmekosa masaa nyie sio bure. Kama mnaipenda sana zanzibar rudini

Anonymous said...

Tumechoka na ujinga wa ZADIA. Watu tupo busy kuchapa kazi na kulea Familia zetu hapa Marekani. Hatuna muda wa kupoteza na hizo propaganda zenu za kitoto. Mkitaka media coverage, mjiunge na bwana Trump, au mrudi makweni Zanzibar/Pemba mkaandamane!

Anonymous said...

Wakeleketwa,Wenye kujiajiri na wenye flexible schedule wataandamana, wewe usijali.
Kila kitu kina mwanzo.
Hapa kazi tuuuuu!

Anonymous said...

Kabisa true hawa zadia wachunguzwe na propaganda zao

Anonymous said...

Kutangaza matokeo gani? To the best of my recollection the election in Zanzibar was nullified! Hawa ni Wanzanzibari ama Wanachama wa CUF? The two are not necessarily the same.

Anonymous said...

Wanzanzibar wanaoishi nje ya zenji majority ni cuf members.wanapotosha Sana watu hawa na sijui wanamchango gani kwa Zanzibar Kati ya kuleta habari za upotoshaji. Wapemba wana balaa Kweli hawa

Anonymous said...

ZADIA to my knowledge nilifikiri ni Taasisi huru amabayo haikutakiwa kujiingiza kwenye siasa.Kwa mshangao imepoteza mwelekeo na kujikuta ikifanya kazi za upinzani badala ya kujikita kwenye kusaidia kuleta maendereo nyumbani....Hivi kwa nini mnachanganya mambo badara tu ya kujiondoa kwenye Diaspora na kuweka wazi kuwa nyinyi ni Tawi la CUF ? Mngekuwa na mapenzi ya Kweli ya Zanzibar mngeludi sio kukaa mkababaisha watu kwenye mgongo wa Zanzibar Diaspora(ZADIA).Maandamano yenu ni upuuzi na wenye nchi wanaelewa mnachokifanya.....