Sunday, December 6, 2015

Wapambanaji wa ufisadi wazua maswali

UKIMYA wa wanasiasa walioongoza harakati za kupambana na ufisadi katika majukwaa ya kisiasa, wakati huu Serikali ikichukua hatua za wazi na haraka kukabiliana na ubadhirifu wa mali za umma, umeibua maswali kuhusu uzalendo kwa nchi yao.

Miongoni mwa wanasiasa waliohusishwa na maswali hayo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala ya Siasa na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana, alisema kama kweli ni wazalendo, ni vyema wale wote waliokuwa wakipinga ufisadi wajitokeze hadharani, kupongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa.

Profesa Bana alisema hali inavyoendelea nchini kwa sasa ni wazi kwamba Rais John Magufuli, anapaswa kuungwa mkono na wote waliokuwa wakipinga ufisadi na ubadhirifu serikalini. “Ni wakati muafaka sasa wale wote waliokuwa wanapinga ufisadi wakiwemo wanasiasa, wajitokeze hadharani kumuunga mkono Rais wetu, kama kweli walisema hayo kwa uzalendo na uungwana,” alisisitiza Profesa Bana.

Alisema ni wakati sasa wa Sumaye, Lowasa, Mbowe na wengine waliokuwa mstari wa mbele kueleza umma ufisadi na ubadhirifu serikalini kwenye kampeni za kuwania urais mwaka 2015, wakajitokeza hadharani kupongeza kazi inayofanyika.

Pia aliwataka wote waliosema hawataunga mkono serikali iliyoko madarakani, kufuta mara moja kauli yao, kwani yanayoendelea kufanywa ni mambo mazuri kwa ajili ya ustawi wa Watanzania wote bila kujali itikadi zao.

Magufuli na Ilani ya Ukawa “Yapo maneno kwamba Rais Magufuli anatekeleza ilani za vyama vingine na si ya CCM, haya maneno yapuuzwe ni kukosa hoja, ilani za vyama vyote vya siasa vinavyojitambua, zinajibu maswali haya ya wananchi,” alisema Profesa Bana.

Akifafanua hilo, Profesa Bana alisema kuna maneno yanaendelea kuzunguka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu au kwenye mitandao ya kijamii, kuwa Dk Magufuli anatekeleza ilani za vyama vingine vya siasa na kusisitiza hoja hiyo haina mashiko.

Alisema Dk Magufuli anatekeleza yale aliyoahidi kwenye kampeni alipokuwa akiwania nafasi hiyo, kwa kuwa yapo kwenye Ilani ya CCM, huku akisisitiza kuwa ilani za vyama vya siasa mwaka huu zilifanana kwa njia moja au nyingine.

“Sisi tulipata bahati ya kusoma na kuchambua ilani za vyama vitatu CCM, Chadema na ACT-Wazalendo, tulipopitia ilani za vyama hivyo na vingine vilivyoshiriki kwenye uchaguzi uliopita, tulibaini zote zinafanana,” alisema Profesa Bana.

Alisema kama kuna chama kinasema ilani inayotekelezwa ni yao, wangekuwa mstari wa kwanza kujitokeza hadharani kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kutekeleza hayo, lakini kukaa kimya kunazua maswali mengi. Wajuta kutompa kura Alisema ni vyema Rais apewe nafasi aendelee kutekeleza anayofanya kwa sababu anajibu maswali ya wananchi yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu na kwamba wapo baadhi ya wananchi wanajuta hivi leo kwa kutompigia kura.

“Tunazungumza na watu mbalimbali wanatuambia wanajuta kumnyima kura Rais Magufuli, kwa sababu kama asingeshinda, nchi ingekosa kiongozi mzuri na mwenye kasi ya maendeleo kwa wote,” alisema Dk Bana.

Wapenda utajiri Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Profesa Kitila Mkumbo alitoa mwito kwa Watanzania wote kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kubadilisha mitazamo yao ya kupenda vya bure, bali wafanye kazi kwa bidii. Profesa Mkumbo alisema juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli, zitakuwa na tija zaidi iwapo Watanzania wote watamuunga mkono kwa kubadilisha mitazamo yao ya kupenda utajiri wa haraka haraka.

“Jitihada za Rais Magufuli pekee hazitoshi, bali jamii yote ya Tanzania lazima ibadilike, tuache kufanya vitu kwa mazoea na kupenda vya bure na utajiri wa haraka haraka, bali tupende kufanya kazi kwa bidii,” alisema Profesa Mkumbo.

Alisema masuala ya ubadhirifu na ufisadi ni mambo sugu yanayosumbua nchi na hatua zilizoanzwa kuchukuliwa na Rais Magufuli ni nzuri kwani tofauti na serikali zilizopita, yeye anatekeleza kwa kasi zaidi.

“Ubadhirifu ni tatizo sugu nchini, lilianza kufanyiwa kazi tangu enzi za Mwalimu Nyerere hadi Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ila kwa awamu hii ya Rais Magufuli, yeye anatekeleza kwa kasi zaidi,” alisema Profesa Mkumbo.

Habari Leo

5 comments:

Anonymous said...

PROF Bana, asante sana kwa maneno mazuri ya utambuzi. Mimi sina upande wa kuegemea sote ni waTanznia. Ni jambo la kushangaza kabisa hata hao wanaCCM wenyewe wameshikwa na butwaa nini kilichoibuka kwani walitarajia kuendelea ale waliyoyazoea ila kwa hali hii mimi namsifu sana Dr JPM na hata nchi nyingine zimeliona na kuliwekea mkazo aendelee hivyohivyo. Hili ni swala la sote waTanzania sio kwamba waliokuwa wapinzani wamekaa kimya au hii habari ya mitandaoni kuwa anafanya kazi ya ilani ya upinzani sio sidhani kama tuko sahihi sana hii ni kazi ambayo waliokuwa madarakani wangelikuw awameifanya sahihi au hata kw akiwango Fulani basi tusingelikuwa tunashangaa! Mfano mzuri tu ni wa hivi majuzi unaoihusisha ESCROW! kwani hakukuwepo na uongozi ila swala hili lilifumbiwa macho na nadhani ni vizuri pia mheshimiwa Rais akalifuatilia ili uhakiki huu ueleweke kwanini UFISADI uliotukuka na kubarikiwa na uongozi wote mzima kuhalalishwa na wahusuika akiwepo mtoaji huduma mwenyewe akiendelea kutesa. hili halikubaliki. Namaliza nikisema mafisadi papa bado wapo na mheshimiwa Rais bado hajaweza kuwagusa kwa kuwa wako na majina makubwa, haya anayofanya ni ya ukwepaji kodi na kutowajibika ambayo yameonyesha faida kubwa bado kuna mengi na hayawezi pekee yake na ndio maana kwenye uteuzi wa mawaziri unampa kigugumizi kwani wale wale wanadhani wataka waendelee kuwepo nchi itaendelea kugubikwa na majanga, hawatakiwi ni vyema awapumzishe. Tanznaia inakuw aya dili tupu na sio utendaji kazi sio wakati wake. viva Dr.Magufuli.

Anonymous said...

benson bana,ama kweli,umesoma lakini una akili finyu akili mbovu,mawazo potofu yaliyojaa ushabiki usio na kupima,mropokaji na umekua unajaribu kuulazimisha utashi wako wa kisiasa[ambazo umejaa nadharia yake tuu].jaribu siasa benson katika chaguzi zijazo ugombee hata ujumbe wa nyumba 10 wa ccm,uingie ndani ya siasa.kwa sasa unaeneza unafiki wako tuu.unaposema mhe.lowassa na mbowe wajitokeze hadharani kupongeza kinachoendelea kuhusu mhe.magufuli kufuatilia wizi mkubwa wa makontena bandarini,utendaji mbovu wa hujuma kwenye mashirika yetu,lawama zooote ni kwa utawala wa ccm wa awamu ya nne. kwa nini husemi kikwete aanze kuhojiwa kwa hatua za kisheria?unamlinda.hizi ni dhambi za ccm na mhe.magufuli anapambana na madhaifu ya mtangulizi wake.ni mpaka hapo atakapoletwa kwenye vitabu yaani ASHITAKIWE NDIPO UKAWA TUTAPONGEZA.sasa hivi ni mtifuano tuu kwa vidagaa mapapa wanastarehe kama vile hakuna kitu.bana jifunze akili nzuri,acha akili za uccm.

Anonymous said...

Wewe ndiyo una akili finyu kwani hujui hata kuandika. FISADI.

Anonymous said...

Dr. Bana umenena. UKAWA wameduwaa silo CCM kwa sababu Mheshimiwa Rais anatekeleza ilani CCM kama alivyojinadi wakati wa kampeni kwamba atapambana na ufisadi na ubadhirifu. UKAWA hawakuthubutu kutamka hilo wakati wa kampeni "for obvious reasons". Kutukana mtoa hoja nido ufinyu wa akili kupindukia. Asamehewe tu bure. Mhehsimiwa Rais tuko nawe na hatuoni aibu kuitetea CCM na kukusifu kwa kazi nzuri unayoifanya kwa niaba ya chama chetu. Hkuna kitu rahisi kama kulaumu. Unaweza kufanya vile hata ukiwa umelala chini au unashinda mitandaoni kuandika tu porojo!!

albert said...

kIUKWELI NAWEZA KUSEMA SAWA WASOMI LAKINI VITU VINGINE WANAVYO ZUNGUMZA SIFIKIRII KAMA NI VYAKISOMI, SASA HUYU MZEE ANAPOSEMA WANYANYUKE WALE WAPINZANI WAKE INAMAANA HAKUMWELEWA RAIS MAGUFULI ALIVYOSEMA SIASA SIMEKWISHA SASA NI KAZI? AU NATAKA KULETA MIPASHO? MTU KAZI YAKE KWA SASA NZURI HAINA UBISHI, ATAKAE MPINGA NI CHIZI TU, MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KUPINGA KAZI ANAYO FANYA MAGUFULI, BARAZA LA MAWAZIRI LIMECHELEWA HAKUNA MPINZANI KAHOJI, SABABU WANAAMINI ANACHOKIFANYA, AU NAOMBA NIMUULIZE BANA ALITAKA WAPINZANI WAZUNGUMZE NINI HASA, HARAFU HUYU MZEE NAONA ANAMATATIZO KIDOGO, HAYA ANAYO FANYA RAIS SINDIO YALIKUWA YANAPIGIWA KELELE NA WAPINZANI? AU HUU UOZO WALIUFANYA WAPINZANI? ASILETE MIPASHO KWENYE ISHU YA KUJENGA NCHI, MSIGWA ALISHA SEMA, TUSIRUHUSU AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, LEMA ALISHASEMA HAWAGOMBANI NA CCM BALI WANAWAKUMBUSHA KUWAJIBIKA, NA WAKIFANYA VIZURI SAWA HATA WAKITAWALA MIAKA 1000 SAWA HAINA SHIDA, SASA BANA WEWE NI NANI HAPA, UNATAKA WASEME NINI WAPINZANI