Friday, January 22, 2016

AHUKUMIWA MIAKA 19 JELA KWA KUIBA MBUZI MKOANI MBEYA

Na Ezekiel Kamanga,,Mbozi.

MAHAKAMA ya mwanzo vwawa mjini wilayani Mbozi mkoani Mbeya imemuhukumu Patrick Moses(19) mkazi wa Ilembo  kutumikia jela miaka mitano baada ya kukiri kosa la kuiba Mbuzi mmoja mwenye thamanai ya Sh 85,000 mali ya Bahati Mtafya.


Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama hiyo,lazima Mwaijega alisema kutokana kifungu cha sheria 268 na mshitakiwa kukiri kosa hivyo mahakama imeamuru mshitakiwa kutumikia kifungo hicho ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.

Mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia yake,hata hivyo hakimu Mwaijega amesema kifungo hicho cha miaka mitano amepunguziwa pia kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na kwamba.

Awali imeelezwa mahakamani na  mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa January 20,mwaka huu saa 11 jioni  mshitakiwa alivamia nyumbani kwa Bahati Mtafya (38) na kuiba mbuzi mmoja mwenye thamani ya Sh. 85,000 huku akijua kufanya vyo ni kosa kisheria namba 229 sura ya 16 kanuni ya adhabu.

Aidha mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wale wenye nia ya kutendakosa kama hilo kutokana na wimbi kubwa la vijana kujikita katika wizi na kuacha kufanya kazi halali.

Katika hatua nyingine mshitakiwa huyo alipandishwa kizimbani hapo kujibu tuhuma ya wizi wa kuku 23 wenye thamani ya Sh laki 4 mali ya Evance Mwakenja mkazi wa Ilembo Vwawa 

Imeelezwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa tukio hilo lilitokea januari 20 mwaka huu saa 8 usiku ambapo mshitakiwa aliiba kuku 23 wenye dhamani ya Sh.laki 4 mali ya Evance Mwakenja huku akijua kufanya hivyo nikosa kisheria.

Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka linalomkabili na hakimuwa mahakama hiyo Chirstina Mlwilo amesema shauli hilo litaanza kusikilizwa Januari 27 mwaka huu,pia hakimu huyo amesema dhamana kwa mshitakiwa ipo wazi kwa ahadi ya Sh.laki 4 pamoja na kuwa na  wadhamini wawili wenye vitambulisho vya mpiga kura. 

 Hata hivyo mshitakiwa ameludiswa maabusu kwa kushindwa kutimiza masharti  la dhamana pamoja na kuanza kutumikia kifungo cha miaka mitano ya wizi wa mbuzi.
mwisho.
JAMIIMOJABLOG

4 comments:

Anonymous said...

JAMANI KUNA WENYE MAKOSA ZAIDI YA HILI, THAMANI YA MBUZI NI SH NGAPI, NA GHARAMA YA KUISHI KWAKE JELA SH NGAPI!!!! WEWE JADGE UMESOMEA WAPI!! HUYU MFUNGWA AKIUGUA ATATIBIWA KWA ZAIDI YA HII PESA YA MBUZI.KULA,KULALA,NI GHARAMA ZAIDI YA HUYO MBUZI YAANI NI HASARA KWA KODI ZA WANANCHI.

Anonymous said...

TOO BAD, INJUSTICES IPO HATA BONGO? MIAKA MITANO KWA KUIBA MBUZI, WAKATI MAFISADI WANAIBA MAMILIONI NA WANAFUNGWA ZERO DAYS? TAFADHALI BUNGE MKAE CHINI NA KUREKEBISHA SHERIA ZA MAHAKAMA ILI HUKUMU ZIENDE SAMBAMBA NA UZITO WA MAKOSA. ALSO, HUYU JAJI SHOULD HAVE SHOWN MERCY, GIVEN THE CIRCUMSTANCES. I NOW SEE THE DIFFERENCE BETWEEN JD AND LLB.

Anonymous said...

Ni kweli kabisa Mliotangulia. Serikali inabidi iwe Inaangalia hizo Sheria za Mahakama kwa Mapana na Marefu kama hizi. Mafisadi Wanaiba Mali za Serikali na hawachukuliwi hatau yoyote ile! Huyo aliye iba Mbuzi ana Familia inayomtegemea, Judge haoni kwamba Kifungo hicho kitawaathiri Familia yote??. Kwanini msimwambie alipe hiyo Thamani ya Hela zilizotajwa tu au Arudishe huyo Mbuzi kwa Muhusika?? Huyo Judge anatakiwa awe na roho ya Ubinadamu. Period!!

Anonymous said...

Mtu asiyekubaliana na hii adhabu atuambie sheria inataka adhabu gani itolewe kwa kosa kama hili. Msituambie wengine wameiba mamilioni, lakini hawajafungwa; hiyo siyo kazi ya hakimu au judge! Hakimu au judge akiendesha kesi kwa mtindo huo, hakuna mkosaji atakayeadhibiwa. Wapo mahakimu na majaji wengi ambao wamehukumu wengi kwa makosa ambayo mahakimu au majaji wenyewe wamewahi kuyafanya na wengine wanaendelea kuyafanya, kama vile kupokea rushwa. Kimsingi, kazi ya hakimu au judge ni kupima hoja na ushahidi ulioletwa mbele yake na kisha kutafisiri matakwa ya sheria, katika kufikia uamuzi wake!

That there are so many more serious crime perpetrators out there, who remain free, is irrelevant! If you don't like the law and the law enforcement, tell your corrupt legislators to fix them; it's that simple!