Sunday, January 3, 2016

Balozi Seif afanya usafi kwenye uzunduzi wa sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishiriki na Wananchi, Vikundi ya vya usafi wa mazingira pamoja na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafi wa mazingira hapo Kwahani Uwanja wa Farasi ikiwa ni kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 196. 

 Picha na – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira Mwenyekiti wa Kikundi cha Usafi wa Mazingira cha Kilimani { Kilimani City } Nd. Khamis Shaali Chum { mwenye T. Shirt Nyeupe }vilivyotolewa zawadi na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira.Kushoto ya Mwenyekiti huyo wa Kilimani City ni Mkurugenzi Maingira Nd. Juma Bakari Alawi na wa kwanza kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja.
Baadhi ya wapiganaji wa Vikosi vya ulinzi wakishiriki zoezi la usafi wa mazingira katika Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi kuanza kwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52.
Watendaji wa Baraza la Manispaa Zanzibar wakijumuika pamoja na Wananchi na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafishaji wa mazingira hapo Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi Mjini Zanzibar.

2 comments:

Anonymous said...

Kwa mujibu wa katiba huyu jamaa sio makamu wa Rais tena jamani

Anonymous said...

Kwa mujibu wa katiba huyu mjamaa siyo makamu wa Rais tena jamani!!!