Friday, January 22, 2016

DK SHEIN ASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UWT KATIKA KIJIJI CHA KIANGA WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein (watatu kulia) akijumuika na Viongozi wengine wakiwa katika mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar, Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kianga wakati wa mazishi hayo leo asubuhi. wa pili kulia ni Baba Mazazi wa Marehemu Asha Bakari Makame Mzee Bakari Makame.
VIJANAS wa Chama cha Mapinduzi wakiwa amebeba jeneza likiwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari Makame wakati wa maziko yake katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi B Unguja leo asubuhi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Viongozi wa Serikali wakishiriki katika Mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kijiji cha Kianga nje kidogo ya Mji wa Unguja Wilaya Magharibi B.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwaka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Asha Bakari Makame.
MAKAMU wa Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal akiweka mchanga katika kaburi.
BABA Mzazi wa Marehemu Mzee Bakari Makame akiwaka mchanga katika kaburi la mwanawe baada kuzikwa katika makaburi ya Kianga Kijijini Wilaya ya Magharibi B Unguja
WANANCHI wakihughuria mazishi ya Marehemu Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Asha Bakari Makame katika makaburi ya Kianga Wilaya ya Magharibi B Unguja leo asubuhi.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akisoma wasifu wa Marehemu Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Asha Bakari Makame wakati wa mazishi hayo yaliofanyika katika makaburi ya Kianga nje kidogo ya Mji wa Unguja Wilaya ya Magharibi B Unguja.(Picha na Ikulu, Zanzibar)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake