ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 7, 2016

DK. SHEIN AZINDUA SKULI MPYA KIJIJI CHA ZINGWEZUNGWE ZANZIBAR.

WA2
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Skuli ya Msingi Mnarani leo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa  kwa  Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar,ufunguzi huo ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar(kulia) Katibu Mkuu Wizra ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi.Khadija Bakari na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna (kushoto).
WA3
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani leo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa  kwa  Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar,ufunguzi huo ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
WA4
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi  mara baada ya kuifungua na kuitembelea  Skuli ya Msingi Mnarani   Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,iliyojengwa  kwa  Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar,  ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
WA5
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mnarani   nbsp;Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kuifungua rasmi leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
WA6
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akipokea Risala kutoka kwa Mossi Hamadi Khamis katika sherehe ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa  kwa ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele Zanzibar Foundation  leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
WA7
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi, pamoja na viongozi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo iliyojengwa  kwa ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele Zanzibar Foundation   ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
WA1
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Wizra ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi.Khadija Bakari wakati alipowasili viwanja vya Skuli ya Msingi Mnarani Wilaya ya Micheweni kuifungua Skuli hiyo iliyojengwa kwa Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar leo ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Na Ali Issa Maelezo –Zanzibar
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haruon Ali Suleiman ameshauri  walimu watakaosomesha Skuli ya Zingwezingwe wawe walimu wanaoishi karibu na  kijiji hicho.
Hayo ameyasema leo huko Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, wakati alipokuwa akifungua skuli mpya ya msingi ya kijiji hicho ikiwa ni miongoni mwa  shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .Ametaka ushauri huo ufanyiwe kazi  na iwapo watahitajika walimu wapya  kuajiriwa kwa  ajili ya kufundisha katika skuli hiyo  Wizara yake   ambayo ndiyo  inayohusika na  masuala ya ajira   watakuwa tayari  kufanya hivyo.
“Ni vyema kuajiri walimu wakaazi  na wenyeji wa kijiji cha Zingwezingwe  wenye kuyaelewa mazingira ya kijiji hicho na mimi kama Waziri wa Ajira niko tayari   kusaidia hilo,” alisema Waziri Haroun.Aidha aliwashauri wanafunzi  wanaosoma  katika skuli hiyo  kuitumia  frusa waliyoipata  kusoma kwa juhudi  kwani hiyo ni skuli ya kwanza  kujengwa katika kijiji hicho.
Hata hivyo aliwataka wazazi  na walezi kwa  upande wao kutimiza wajibu wao  wa kufuatilia kikamilifu maendeleo ya Watoto  wao  na kutoa ushirikiano  kwa walimu ili kufanikisha maendeleo ya watoto wao.
Waziri Haroun  aliwataka walimu kusomesha kwa juhudi kwani serikali  tayari imeshatoa maelekezo ya kuwaongezea maslahi yao  mara itakaporudi madarakani baada ya uchaguzi  wa marejeo.Katika kuongeza ujenzi wa madarasa mengine ya kusomea katika Skuli hiyo, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utawala wa Umma  alichangia matofali 1000 ambapo ujenzi wake utaaza hivi karibuni.
Nae Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Mama Asha Balozi akitoa salamu za Baloz Seif Ali Idd alisema suala la umeme katika skuli hiyo litafanywa na Makamu huyo wa Rais.

 Ujenzi wa skuli hiyo yenye  madarasa  manne na Ofisi ya Mwalimu Mkuu umegharimu shilingi milioni 66 ambazo zimetolewa na  Shirika la Maendeleo la Sweden SIDA, Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B, Mbunge na Mwakilishi na Wazee wa kijii cha Zingwezingwe.

No comments: