ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 11, 2016

JK AMPONGEZA SAMATTA LEO

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiingia ukumbini na Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, alipokutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.Picha zote na Bashir Nkoromo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa ukumbini na Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, alipokutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Kikwete kuzungumza na waandishi wa habari, katika hafla hiyo ya kumpongeza Samatta. 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Kikwete akizungumza na kumpongeza Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta (kushoto), alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.Kulia ni Waziri Nape.
Nyota wa Soka wa Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Kikwete, aliyokuwa akiitumia katika timu ya TP Mazeembe ya Congo DRC, katika hafla ya Kikwete iliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili yaRais huyo mstaafu kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.
JK na Samatta wakitoka ukumbini
Samatta akiongozana na Kikwete kutoka ukumbini huku akiwa na tuzo yake
Samatta akiongozana na Kikwete kutoka ukumbini huku akiwa na tuzo yake
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Kikwete na Waziri Nape wakirudi Ofisini baada ya kumsindikiza Samatta
Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye hafla hiyo leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments: