Saturday, January 23, 2016

Jokate, Kiba wamwagana


Staa wa Bongo, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’.

MUSA MATEJA, Risasi Jumamosi
Dar es Salaam: Hii ni habari ya kipekee (Exclusive Story)! Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wanadaiwa kumwagana, Risasi Jumamosi ndilo gazeti pekee linaloweza kuthubutu kukupa mchapo kamili.

Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wakiwa katika pozi.

Habari ya mjini kwa sasa ni juu ya wawili hao ambao walikuwa gumzo kwa watoto wa mjini, kwa kila mmoja kuchukua hamsini zake na kufanya yake tofauti na walivyokuwa awali huku chanzo cha kutengena kwao kikitajwa kuwa ni wazazi wa sehemu zote mbili kutoridhiana.

Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao, mbali na ishu ya wazazi, hivi karibuni Jokate na Kiba waliingia kwenye gogoro kubwa la kimapenzi baada ya kufumaniana kwenye simu, jambo ambalo limeendelea kutokea huku jamaa akiongoza kukutwa na meseji kwenye simu yake za mwanamke mmoja anayedaiwa kuishi nje ya Tanzania.

BOFYA HAPA KUSIKIA CHANZO
“Ukisema nikusimulie juu ya kumwagana kwa Jokate na Kiba basi tunaweza kukesha ila mbali na mambo ya wazazi, kwa kifupi tu ni kwamba, hawa watu wameingia kwenye mgogoro na kilichokuwa kikiwagombanisha mara nyingi ni uhusiano wao wa zamani.”

KIBA ANA DEMU?
“Mara kadhaa Jojo (Jokate) amekuwa akimlalamikia jamaa (Kiba) kuwa ana demu nje ya nchi ambaye amekuwa akimtundika katika mitandao ya jamii na kujinadi kuwa ndiye mkewe tofauti na wengi wanavyojua kuwa Jokate ndiye mtu wake.

“Mbali na hilo, sasa kuna suala la familia zao kuonesha hali ya kutokubaliana na wao kuoana hasa upande wa Jokate ambao ulionesha msimamo mkubwa kutomtaka hata kidogo Kiba, mambo hayo yamekuwa ni chagizo kubwa katika kuhatarisha mapenzi yao hivyo kufikia hatua hata ya wao kutoendelea kupendana kwa dhati kama ilivyokuwa mwanzo wa penzi lao.”

VIKAO VYAGONGA MWAMBA
“Tofauti na watu walivyozoea kuwaona pamoja, kwa sasa wametibuana na hapa tunapozungumza tayari kuna vikao kibao huko nyuma vilishakaa ili kunusuru penzi lao lakini imeshindikana maana kila mmoja sasa hivi anajifanyia mambo yake na hakuna dalili za kurudiana.

“Kiba anaonekana ameshajiingiza kwenye penzi la demu wake wa zamani huku Jokate naye akiwa ‘in love’ na mtu wake mwingine.”

MPANGO WA KUZAA WAYEYUKA
“Kitambo tu nimekuwa nikiwaambia kwa staili waliyokuwa nayo hakika wasingeoana hata kama ukiweka pembeni suala la dini zao kutoendana, maana kuna siku niliwasikia wakiambiana hata kama wazazi wakigoma wao wangefanya kila juhudi hata wazae pamoja tu.

“Lakini ukweli ni kwamba ilishindikana baada ya kuanza kugombana mara kwa mara, pamoja na kwamba Jokate alikuwa akikubalika kwa asilimia zote kwa mama Kiba na hata ndugu wengi wa Kiba walionekana kumpenda waziwazi,” kilisema chanzo hicho.

KIBA AFUNGUKA
Baada ya kupenyezewa mchongo huo, gazeti hili liliingia mzigoni kumtafuta Kiba ili atoe la moyoni juu ya madai hayo ya kumwagana na Jokate ambapo alipopatikana alisema kuwa haoni sababu ya kuzungumzia ishu hiyo kwani ni mambo binafsi.

“Kusema kweli ishu hii mimi sina uwezo wa kuiongelea zaidi kwa sasa kwani ni mambo binafsi sana na sioni faida ya kuzungumzia vitu ambavyo havina maana.
“Kwanza sioni nini cha kuongelea hapa kwani kila jambo lina mipaka yake,” alisema Kiba akikataa kuulizwa zaidi juu ya suala hilo.

JOKATE VIPI?
Kwa upande wa Jokate alipotafutwa kwa siku kadhaa ili azungumzie sakata hilo kwa ufasaha hakupokea simu ya mwandishi wetu hadi gazeti linaingia mitamboni.

PENZI LA JOKATE NA KIBA
Awali zilipovuja habari za penzi la Jokate na Kiba wote walikanusha, kadiri siku zilivyosonga ndivyo walivyozidi kuwa gumzo kwa mashabiki wao waliofurahishwa na ‘kapo’ yao huku wakionekana kwenye viwanja mbalimbali vya starehe wakiwa kimahaba lakini sasa mambo yanaonekana kwenda mrama.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake