Wednesday, January 6, 2016

Kutokana na Malumbano Yao Mitandaoni, Mzee Yusuf Asema Haya Kwa Wake Zake


Jana ilikuwa siku ya kuzaliwa Mzee Yusuf,kumekuwa na malumbano ya mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kati ya wake zake wawili Leila na Chiku, Mzee Yusuf amesema hafurahishi na malumbano hayo…
‘’Sio vitu vizuri sifurahii huwa najaribu kuwaaambia sijui hawa wake zangu wananionaje ,pengine hawajui kuwa mimi ni mume wao hawanipi heshima yangu na hasa huyo anayetaka kufanya mambo ya vituko,binafsi sipendi na huwa sifurahii na najaribu kuwaasa tena kwenye Instagram huwa nawaambia waangalie hao mashabiki wao ‘maandazi’ lakini sasa unakuta mtu mwenyewe anapenda mambo hayo sasa itafika siku nitakuja kufanya kitu na asije mtu akalalamika,’’alisema Mzee Yusuf.

cloudsfm

2 comments:

  1. ndio tatizo la wake wawili hilo hapo mzee anajionaa eeh napendwa mie kumbe anawaumiza wenzie tuu

    ReplyDelete
  2. Cha kugombania hapo sikioni!!!

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake