Wednesday, January 6, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 6, 2016.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 6, 2016.
Katika Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Kikwete amemtakia Rais Magufuli heri ya Mwaka mpya na kumpongeza kwa uongozi mzuri.
Rais Kikwete pia amesema anaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
06 Januari, 2016. 

5 comments:

  1. It is a good gesture, as long as he doesn't dictate to him what or what not to do. Of course, JPM has fired many of Jk favorites, and I am convinced some have complained about the firing. Frankly, I doubt if it sits well with JK. However, at the end of the day, Magufuli will make the final call.

    ReplyDelete
  2. I believe JK as the he still the party chairman can feel like he has the power to lead the country, and he might be in process of convincing JPM to what to or not to!! Don't just take it easy friend! CCM is something and you will se the situation in ZANZIBAR they are going to do what they did in Bara!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Alienda kuomba kibali cha kutokea na pesa.mkishasikia tra wamekusa ya 14m

      Delete
  3. Tumesikia JK ameenda kupumzika huko Msoga, Sasa mara yupo Ikulu mara Lumumba. Naona ingependeza kama angemwachia JPM uenyekiti wa chama ili mzee akapumzike kijijini kwake apate heshima. Ni vizuri rais aliyepo apewe madaraka ya kuamua anayoyaona kuwa ni mazuri na ambayo yanafanywa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu, JK yeye ameshamaliza kipindi chake.....Tunamshukuru kwa aliyoyafanya amwachie mwenzake awe huru.

    ReplyDelete
  4. Kikwete blah blah blah watanza nia, hamuwachi udaku usio na mshiko kwani Magufuli alipokuwa waziri wake wa ujenzi kikwete alikwenda kumshika mkono na kumwambia magufuli fanya hivi. Maghufuli alifanya kazi kwa bidii bila ya kuingiliwa na raisi. Nna imani kabisa kikwete ni mtanzania halisi na Magufuli si mtanzania sijui tu ilikuwaje kumpata mtanzania kiongozi kama maghufuli mwenye hulka ya uwajibikaji wa nchi za kigeni hasa zile zilizopiga hatua ya kimaendeleo. Watanzania wengi wanaomsemea ubaya kikwete ndio hao hao wanaolalamika kubomolowa nyumba zao kwa kisa kosa la kwenda kununua waraka feki ilihali akijua kuwa eneo analoliombea waraka ni marufuku kujengwa. Watanzania tunataka mabadiliko ya kweli basi tushikane na magufuli kisawa sawa na tusahau yaliopita kwani kiukweli kikwete hakuwa mzembe hata kidogo bali uzembe tatizo liloigubika jamii ya watanzania. Kufikiria short cut, njia ya mkato ili kujipatia mali. Wakati ukweli kwenye maisha halali na halisi hakuna njia ya mkato. Hao ndugu zetu walikuwepo huko nyumbani wakeshakuwa na mtu katika familia yupo nje watu wote hawataki kufanya kazi wanasubiri mkwanja kutoka nje uendeshe maisha yao. Mtumishi wa serikali akiwa na nyazifa kidogo basi asipoiibia serikali jamii yake iliomzunguka inamshangaa na kumuona mjinga. Mtumishi wa ndani wa nyumba akiwa wa kiume asipomfanyia mabaya mke wa bosi wake vijana wenzake wanamuona mpumbavu ee! Vile vile baba mwenye nyumba asipomfanyia vibaya house gali wake anaonekana mzembe jamani? Sasa kaja magufuli awe ndio our new year resolution kwa kukusudia kuondokana na uzembe na watanzania tuwe mfano Africa na duniani kote.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake