Monday, January 4, 2016

MAHAKAMA KUU KITENGO CHA ARDHI KUTOA UAMUZI KESHO KUHUSU OMBI LA ZUIO LA BOMOABOMOA.

Mahakama kuu kitengo cha ardhi kutoa uamuzi januari tano mwaka huu wa maombi ya wakazi wa kata tatu zilizopo wilaya ya Kinonondoni juu ya kuomba zuio la serikali kusitisha zoezi la bomoabomoa.
Kesi hiyo ya kupinga bomoabomoa ya nyumba zilizojengwa kinyume na taratibu ilifunguliwa na mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia ambapo ilikuwa ianze kusikilizwa lakini ikakwama kufuatia mabishano ya kisheria kati ya mawakili wa serikali wanaoisimamia na wakili wa upande wa walalamikaji.
Kesi hiyo namba 822 ya mwaka 2015 inasikilizwa na jaji Penterine Kente ambapo pande zote mbili zilianza kutoa maelezo ukianza na upande wa wakili wa serikali Gabriel Malata ambaye mbele ya jaji Kente amekiri kupokea nakala ya maombi na kuongeza kuwa baada ya kuyasoma wanakusudia kupeleka kiapo kinzani dhidi ya maombi hayo.
Aidha wakili malata ameieleza mahakama hiyo kuwa kutokana na maombi hayo kupelekwa chini ya hati ya dharura na wao watapeleka siku chache zijazo huku akiitaka mahakama hiyo kutokusitisha zoezi hilo kwani sababu za msingi wanazo.

Kwa upande wa wakili wa wapeleka maombi Aboubakary Salum amesema hawana pingamizi na ombi la upande wa serikali kupeleka kiapo kinzani ila wanachoiomba mahakama hiyo ni kusitisha zoezi hilo la bomoabomoa wakati usikilizwaji wa maombi hayo yanaendelea.
Baada ya jaji Kente kusikiliza pande zote mbili amesema maamuzi juu ya maombi ya pande zote mbili kuhusu kusitishwa kwa zoezi au la yatafanyika januari tano mwaka huu na kuutaka uapnde wa serikali kupeleka hati kinzania kabla ya tarehe nane mwezi huu.


CHANZO: ITV TANZANIA

3 comments:

Anonymous said...

Kwa mwendo huu itakuwa ndoto kwa Tanzania kupata maendeleo ya haraka kama tutakuwa tunaingiza siasa katika mambo ya msingi.

Anonymous said...

Kwanza kabisa napenda kuanzia na kusema maeneo mengi ya wazi nchini yalivamiwa kwa baraka za CCM
Wanainchi walianza na kufunguwa matawi ya wakelekwetwa wa CCM viongozi wakuu wa ccm walifunguwa matawi haya kwa vishindo
Watu wa kaanza kujenga sehemu hizi hasa Jangwani Dar , yakawa ni mazoea mafuriko yakitokea missada inatoka serikali ya ccm ikawa inatumia mabilion ya fedha , Tanzania tuna sehem kubwa sana ya watu kuuishi sasa kwanini wasitengeze maandalizi kwa watu hawa?
Kabla , Kama ni uvamizi ccm ni namba moja maeneo mangapi nchini yalikuwa wazi CCM imejenga ofisi zao.
Nafikiriki hata hayo mahekalu ni kulipiza kisasi tu ,
Yatawagharimu sana haya ccm

Unknown said...

Maamuzi ya leo mahakama ni nini juu mgogoro huu nijuze