ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 26, 2016

MAHAKAMA YATOA SIKU 6O KWA WAKAZI WA MABONDENI KUJITATHMINI KAMA WANAWEZA KUFUNGUA KESI YA MSINGI

Baadhi ya wakazi wa bonde la Kinondoni Mkwajuni wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi wakisubiri maamuzi ya mahakama hiyo ya kesi yao ya kupinga kubomolewa nyumba zao. Hata hivyo katika maamuzi yake mahakama hiyo ilitoa siku 60 kwa wakazi hao kujitathimini kama wanaweza kufungua kesi. (Picha na Loveness Bernard).
 Mbunge wa Kinondoni akizungumza na wakazi wa mabondeni nje ya mahakama hiyo.

Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia akiagana na wananchi waliobomolewa nyumba zao ambao walifungua kesi ya kupinga zoezi bomoabomoa.


MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Ardhi, jijini Dar es Salaam imetoa uamuzi wa siku 60 wa kusimamamisha mchakato wa bomoa bomoa kwa wakazi wa mabondeni zaidi ya 600 ili wajitathimini kama wanaweza kufungua kesi ya msingi dhidi ya Serikali.

Uamuzi huo ulitolewa jana mahakamani hapo na Jaji Penterine Kente, kuhusu maombi ya wakazi hao kutobomolewa nyumba zao pamoja na kutaka kufungua kesi ya msingi.

Shauri hilo namba 822 lilifunguliwa na watu saba wakiwawakilisha wenzao 674 dhidi ya Manispaa ya Kinondoni, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (Nemc) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika uamuzi huo uliochukua takribani saa moja, Jaji Kente alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, mahakama imelikubali ombio hilo la kufungua kesi ya msingi, lakini wananchi hao wanapewa siku hizo kwa ajili ya kujitathmini kama wanaweza kufungua kesi hiyo ama lah.

Alisema hatua ya kutoa uamuzi huo unatokana na mahakama kufuata misingi ya Haki na ubinaadamu kutokana na wakazi hao kushindwa kutimiza baadhi ya masharti yaliyotolewa.

Akibainsiha masharti hayo, Jaji Kente alisema la kwanza ni kuhusu waombaji hao kama wanaonyesha wana kesi dhidi ya serikali, pia kama kuna uzito wa kufungua kesi hiyo kwa misingi ya haki kwamba inaangukiwa wapi sambamba na waombaji hao kama watapata hasara isiyopingika.

No comments: