Friday, January 22, 2016

Membe amkosoa Magufuli

By Kizitto Noya, Mwananchi

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali iliyopita, Bernard Membe ameungana na waziri mwenzake wa zamani, Dk Makongoro Mahanga kukosoa sera ya kubana matumizi ya Rais John Magufuli ya kudhibiti safari za nje na kuteua baraza dogo la mawaziri.

Kama ilivyokuwa kwa Dk Mahanga, waziri huyo aliyedumu kwa miaka tisa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje amesema kiuhalisia, Rais hajapunguza idadi ya wizara kama alivyosema bali amepunguza “idadi ya mifuko”, huku akisisitiza kuwa mkuu huyo wa nchi atalazimika kutoka nje “atake asitake”.

Membe amekuwa waziri wa pili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kukosoa sera ya kubana matumizi ya Serikali ya Awamu ya Tano baada ya Dk Mahanga, ambaye sasa amehamia Chadema, kumkosoa akisema idadi ya wizara inapimwa kwa kuangalia makatibu wakuu na si wizara na hivyo ukubwa wa Baraza la Mawaziri bado uko palepale.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi mapema wiki hii, Membe alikuwa na maoni kama hayo na akaenda mbali zaidi kuzungumzia hata sera ya kudhibiti safari za nje na Rais kujizuia kusafiri, akisema “Tanzania haiwezi kuishi kama kisiwa” katika dunia ya leo.

Kubana matumizi


Membe, ambaye alikuwamo kwenye kinyang’airo cha urais na kufika hadi tano bora, alisema Rais hajabana matumizi yoyote kwa kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, bali alichofanya ni kupunguza idadi ya mawaziri na siyo wizara.

“Alichofanya ni sawa na kuwa na mayai kumi halafu ukaamua kuyaweka kwenye mifuko kumi, maana yake ni kwamba utakuwa na mifuko kumi yenye mayai,” alisema Membe.

“Lakini unaweza kuwa na idadi hiyo hiyo ya mayai na ukaamua kuyagawanya; mayai matatu unayaweka kwenye mfuko mmoja, mawili kwenye mfuko mwingine na yaliyobaki kwenye mfuko mmoja. Maana yake ni kwamba utaendelea kuwa na mayai kumi lakini idadi ya mifuko imepungua. Hapa sasa utakuwa hujapunguza gharama za kuyatunza hayo mayai.”

Rais aliahidi kwenye kampeni na hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge kuwa atapunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri ili kubana matumizi. Alitekeleza ahadi yake kwa kuunda baraza lenye mawaziri 34 tofauti na lililopita ambalo lilikuwa na mawaziri 55.

Upunguzaji huo wa baraza ulifanywa kwa kuunganisha wizara na hivyo kufanya makatibu wakuu, ambao ni maofisa masuhuli wa wizara kuwa zaidi ya mmoja kwenye baadhi ya wizara.

“Ameendeleza wizara zilezile, lakini akaamua kuzikusanya pamoja. Hiyo haimaanishi kuwa atakuwa amepunguza gharama za uendeshaji wake,” alisema Membe.

“Hilo tutaliona kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka huu. Tuone kama bajeti itaongezeka au itapungua? Kwa sababu kama wizara zimepungua kama tunavyoamini, lazima bajeti ipungue, sasa bajeti ikiongezeka au ikibaki vilevile maana yake hakuna kilichofanyika.”

Membe alitoa mfano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo sasa inaitwa “Wizara ya Mambo ya Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Afrika Mashariki”, akisema itapaswa kuwa na bajeti mbili; ya Mambo ya Nje na Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kinyume chake ni vigumu kuiendesha.

Membe alikiri kuwa hata yeye angeingia kwenye mtego wa kupunguza idadi ya wizara kama angefanikiwa kuchaguliwa kuwa Rais kama ilivyokuwa nchini Namibia ambako wizara zilipunguzwa kutoka 32 hadi 20.

“Baadaye nikagundua kuwa hata Namibia yenyewe inajuta,” alisema.

Alisema siku ya kuapishwa Rais Magufuli, alikutana na Makamu wa Rais wa Namibia, Nickey Lyambo na baada ya kusalimiana na kumpongeza kwa hatua ya kupunguza wizara, kiongozi huyo wa Taifa hilo la kusini mwa Afrika alimweleza kuwa uamuzi huo umewasababishia matatizo makubwa bungeni

“Aliniambia katika Bunge la Namibia kuna mjadala mkali wa kutaka wizara ziongezwe,” alisema Membe akimnukuu makamu huyo wa rais wa Namibia.

Membe alibainisha kuwa kwa Tanzania, mfumo huo mpya wa wizara pia unaweza kuathiri uwasilishaji wa bajeti bungeni kwa kuwa mawaziri sasa watahitaji muda mwingi zaidi kuliko ilivyokuwa awali ili kuzungumzia wizara kadhaa zilizounganishwa, jambo ambalo lililalamikiwa pia na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu. “Kila kitu kina form na content (muundo na maudhui). Alichofanya Rais Magufuli ni kubadili form na siyo content ya wizara, wizara ni zilezile na mzigo ni uleule,” alisema.

Safari za nje

Mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi, pia alikosoa udhibiti wa safari za nje, akisema Tanzania si kisiwa.

Alikuwa akijibu swali lililomtaka aeleze uhalisia wa mpango wa Rais Magufuli kubana matumizi kwa kufuta safari za nje za mawaziri na watumishi wengine wa umma.

Mara tu baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alifuta safari zote za nje ya nchi kwa watendaji na watumishi wa umma, isipokuwa zile tu ambazo zingepata kibali cha Ikulu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kubana matumizi ya Serikali.

Rais Magufuli alisema katika hotuba yake ya kuzindua Bunge kuwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2015, safari hizo ziliigharimu Serikali Sh356.3 bilioni na kwamba kati ya fedha hizo, Sh183.1 bilioni zilitumika kwa ajili ya tiketi za ndege, Sh68.6 bilioni kwa ajili ya mafunzo na Sh104.5 bilioni kwa ajili ya posho.

Bila kugusia madhara ya kufuta safari hizo, Rais Magufuli alijielekeza zaidi kwenye matumizi ya fedha ambazo angeokoa.

“Lakini tujiulize fedha hizo zingeweza kutengeneza zahanati ngapi? Zingeweza kutengeneza nyumba za walimu ngapi? Zingeweza kutengeneza madawati mangapi? Zingeweza kununua dawa hospitalini tani ngapi?” alihoji Rais Magufuli katika hotuba yake iliyotoa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Lakini Membe, ambaye wizara yake iliwahi kutetea safari za Jakaya Kikwete nje ya nchi baada ya wapinzani kusema ziligharimu zaidi ya Sh4 trilioni, alisema safari za nje zina umuhimu kwa taifa lolote.

“Tanzania si kisiwa, hata ukiwa tajiri namna gani lazima utoke nje ya nchi yako,” alisema Membe ambaye ana shahada ya umahiri ya uhusiano wa kimataifa aliyoipata Marekani.

“Lazima utakwenda mwenyewe au mawaziri wako na hasa Waziri wa Mambo ya Nje kwa sababu kuna vikao nje ya nchi ambavyo mabalozi hawaruhusiwi kuingia.

“Ukijaribu kujifanya kisiwa utakuwa kama Zimbabwe. If you isolate yourself you will be isolated (ukijitenga, utatengwa).”

Membe alisema nchi ina mabalozi 36 tu duniani kote kati ya nchi 194 zinazohitaji uwakilishi huo na kibaya zaidi, mabalozi hawaruhusiwi kuingia kwenye baadhi ya vikao, na hata wakiingia wakifika kwenye hatua ya uamuzi watazuiwa kushiriki.

“Kwa mfano, Uturuki hatuna ubalozi, sasa unapoona ndege inaleta watalii kutoka Uturuki, unadhani Bunge la Uturuki liliketi kutuletea watalii Tanzania? Hapana. Tulitoka nje na kuwashawishi wakaja,” alisema Membe aliyewahi kueleza kuwa wakati wa awamu ya Rais Jakaya Kikwete mawaziri walikuwa wanapishana angani kana kwamba kuna moto ardhini.

“Pia, leo unaposikia gesi, gesi, gesi nayo imepatikana nje ya ubalozi. Mawaziri walitoka nje ya nchi wakatafuta wawekezaji. Ni kazi ya wizara kufanya yote hayo.”

Membe alirudia kauli aliyoitoa siku chache kabla ya kuanza mchakato wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana kuwa lazima waziri wa mambo ya nje awe nje ya nchi kwa muda mwingi na ikitokea yuko ndani ya nchi kwa mwezi mmoja mfululizo, lazima ni mgonjwa.   

26 comments:

Anonymous said...

utupishe na utuache na Rais wetu!!! wewe ulikuwa ndio mshauri wa rais awamu ya nne, na masuala ya kwenda nje wala haukuona tatizo lolote, katika utumiaji wa hela, kuna wakati raisi alikuwa anakwenda marekani kusign msaada wa hela za maendeleo ukawapakia kwenye ndege zaidi ya watu 54, kufanya nini? shopping? au walienda honemoon? kwa gharama za serikali??? hivi ulikuwa na akili kweli wewe? waache washauri wa Dr Magufuri wafanye kazi, kama wewe unaona hawabani matumizi waache, muda wako ulikwisha mfyuuu!!!

Anonymous said...

kutokana na huo ujinga wako ndio maana wala raisi Dr Magufuri hajakupa ubunge wa kuteuliwa!!!! kajipange upya!!!!

Anonymous said...

Hivi huyu Membe katokea wapi? Hebu amuache Magufuli. Rais wa Botswana hajawahi kwenda nchi yeyote. Hasafiri kabisa na nchi hiyo ina utawala bora na maendeleo ya kuigwa.

Wapi umesikia kasafiri Rais wa Angola. Kusafiri Rais sio lazima. Uhuru wa Kenya kila siku barabarani, wametuzidi kipi?

Muacheni Magufuli awe tofauti.

Anonymous said...

Hivi membe anashindwa kufahamu kwanini wabunge wanapendelea wizara nyingi? Its not nuclear science? Wizara nyingi kamati nyingi pia na mshiko mwingi pia!

Amazing that he has suddenly become so regressive only because he lost his bid for the presidency! Indeed, wanasiasa sio watu wa kuamini. We need more tehnocrats than politicians. Thank God for Magufuli.

Anonymous said...

"Lazima waziri wa mambo ya nje awe nje ya nchi siku nyingi ikitokea yupo nyumbani zaidi ya mwezi mmoja huyo ni mgonjwa"! Really? Hawa ndio walikuwa viongozi wa Tanzania?

Membe has lost his mind. I thought the guy was smart. It just shows how much we didn't know some of these dummies running our country?

Anicetus said...


Dr. magafuli hajakatza safari za watumishi wa serikali kusafiri nchi za nche. Alicho kataza ni zile safari za watumishi wa serikali ambazo ni za holela na hazikuwa na manufaa kwa nchi: matumizi mabaya ya hela za Umma . Sisi tuioko nje ya nchi,tumeshangaa kuona mawaziri wanasafiri na ofice yake nzima. Mfano, Presidentt anasafiri na ndege iloyo jaa viongozi wa taasisi nyini nakadalika. Preseident Dr. Maguli management team wanafuata effeicey ya leadership na kukata pale panaponekana ni kwa faida ya Watanzania. Dr. Magauli team ina watu wengi wilioishi nchi za nje sana na wanajua utaratibu wa mambo ya nchi ya nche, kwa mfano katibu mkuu Amabbsor Sefue. Ambassdor Sefue hawezi kudanganywa na anajua mtu anaye safiri anakwenda wapi, ana shughuli gani,na faida zake. Faida za kukata safari za nche zimeonekana tangu Dr. Magufuli alipochaguliwa. Mpaka sasa wnafunzi wanakwenda shule bure, mahospitali yana vitanada na dawa,bababara zina jengwa: maendeleo yameonekana baada ya siku 70. Mr. Membe: kama unataka kusafiri nchi za nche, unaweza bila kutumia pesa za serkali. Good governance starts with good leadership.
Temba

Anonymous said...

Inaonekana mueshimiwa Membe anamatatizo yake binafsi na muheshimiwa raisi. Kwanini muheshimiwa membe hakutoa kauli yeyote aidha ya kupongeza au ya kulaani wakati mueshimiwa raisi anayatumbua majipu yaliyojaa uvundo kama pale bandarini nakadhalika? Pili kama muheshimiwa membe alikuwa waziri wa mabo ya nje kwa miaka tisa aeleze kwanini alishindwa kabisa kuitangaza Tanzania katika jumuia za kimataifa kiasi kwamba hata mbwana samata alipoteuliwa kuwa mchezaji bora wa Africa wa ndani, waafrica na dunia walipata taabu kama kuna nchi Afrika inaitwa Tanzania? Lakini wakati wa uongozi wake muheshimiwa membe kama waziri wa mambo ya nchi za nje ameisababishia Tanzania hasara ya mabilioni ya pesa kwa kutokuwa makini na misafari isiokuwa ya ulazima kwa watumishi wa serikali mungu bariki membe hakupitishwa kuwania uraisi watanzania wangeuvaa mkenge kwanza kabisa sidhani kama Membe angekuwa na ubavu wa kumshinda muheshimiwa Lowasa katika uchaguzi mkuu kwa hivyo CCM wamshukuru sana Magufuli. Kusema kuwa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Tanzania kazi yake ni kudumisha uhusiano mzuri wa kimataifa peke yake ni dhana iliopitwa na wakati kwani kazi kubwa ya wizara yetu ya manbo ya nchi za nje inapaswa kulenga kuitangaza Tanzania kibiashara. Tanzania ina watu wakarimu, Tanzania inavivutio vya Utalii katika chi chache duniani zilizobahatika kuwa nazo. Wamerikani wametengeneza mbuga yao wanaita Serengeti yaani Serengeti feki kama sikosei ipo kule Florida na sasa ni maarufu kuliko Serengeti original na wamerekani ukitaja Serengeti wanajua ni ile iliokuwepo kule Florida how come? Kwa hivyo muheshimiwa Membe asijaribu kunyooshea kidole kibanzi cha mti kwenye jicho la mtu mwingine wakati yeye mwenyewe ana jiti limemganda jichoni. By the way Muheshimiwa raisi hakukataza safari za nje bali safari hizo ziwe na tija kwa watanzania wote na vile vile hali ya kiuchumi ya nchi ikiruhusu na wigo wa safari hizo nao utapanuka kutokana na mahitaji ya nchi. Na wala muheshimiwa Magufuli hakusema kama hata safiri nje ya nchi hapana atasafiri lakini kutokana na umasikini wa watanzania na Tanzania kwa jumla muheshimiwa raisi ameamua kutumia muda wake zaidi katika kituo chake cha kazi yaani Tanzania ili awe karibu na matatizo yanayowakabili wananchi wenzake. Kwa kiasi kikubwa hongera sana Magufuli na tunauhakika ni kiongozi mwenye nia safi kabisa na nchi na kwa kila mabadiliko anayofanya muheshimiwa raisi anafanya kwa kuzingatia maslahi ya watanzania kwa hivyo sapota ya nguvu inahitajika kwa muheshimiwa raisi ili watanzania tuondokane na umasikini.

Anonymous said...

Yaani hata yeye insider hajaelewa kweli ndio awamu ya nne hii ilikuwa mzigo. Kilichokatazwa ni safari zisizo za lazima na ndio maana ni lazima ziwe approved. Kwanini hawa watu hawaelewi? Huwezi ku-spend what you don't have!

Anonymous said...

Membe hajui analoongea sasa hivi. Si ndiyo huyu Membe aliyesema "TULIKUWA TUKIPISHANA KWENYE NDEGE KAMA VILE NCHI INAUNGUA MOTO" Sasa leo anabadilika? Je safari hizo za Kikwete ambazo alikuwa akifutana na Membe zimetusaidia nini zaidi ya kuongeza madeni ya Taifa hadi kufikia Trillioni 40 kutoka trillioni 18 kabla Kikwete hajashika nchi, wakiwa wanatembea na kufanya shopping ya masuti huko nje huku nyumbani watu walikuwa wanaiba kama hawana akili nzuri na kukwepa kodi kwa sana. Haya yote anayoyatumbua Dr. Magufuli leo ina maana Membe na Kikwete walikuwa hawayaoni? Kila mahali kulikuwa uozo siyo bandarini, mahospitalini,TRA, PCCB,Polisi n.k kote kulikuwa kumeoza, Tanzania ilinuka wakati wa Kikwete na Membe kuliko wakati wowote ule.

Anonymous said...

muheshimiwa Membe please sit down,tuachie magufuli wetu afanye kazi yake,yote hayo ni maneno ya mkosaji,watanzania sijui tumerongwa na nani??yaani mtu asipofanya kazi ni shida akifanya kazi ni shida khaaa

Anonymous said...

Hahahaaa navyojua yeye Membe na wenzake walipokuwa wagonjwa ndio hasaa walikimbilia kutibiwa njee inakuwaje leo anasema waziri wa mambo ya njee akiwa hapa nchini yupo kwa matibabu au anamaanisha ameitwa na mganga wake wa kienyeji kuongezewa dawa

Anonymous said...

membe anyamaze tu majipu yake huko Libya na uarabuni yasije tumbiliwa. naambiwa kajamaa ni kabilionea nyuma tu ya lowassa.

Anonymous said...

Ha ha ha! Kama Lowassa kweli. Akitoa dawa anayotumia ya kufanya nywele nyeusi hata yeye kichwa cheupeeee

Anonymous said...

Kweli wendawazimu wengi Tanzania. Ongeza Membe katika idadi hiyo. Hivi haoni yanayoendelea nchini na hata kushukuru juhudi za Mhe Rais. Iwapo haya yanatoka kwa ccm wale wa Ukawa tunaowafahamu watasemaje? Ama kweli kinyongo cha kushindwa na donge la kukosa bado gumu.

Anonymous said...

Afadhali walizuhiliwa hao wazurulaji kutuchuna peza za nchi yetu na kuongeza umasikini wakati wao Uko nje ya nchi walikuwa fanya shoppings......lol!

Anonymous said...

Fisadi mkubwa weeee!!!!!! kwanza mmjilimbikizia mali kila kola, na kujijazia, wakati wengine wanangaika, sijui mwataka kwenda nazo wapi. maanake ni nyingi mno, hamna hata haya, kijuso shuti kimempauka kwa roho mbaya, mweusi mpka na moyo mweusi

Anonymous said...

Sasa hii tabia ya kusafirisafiri mbona ni sisi tu wafrica tena Tanzania ilikuwa inaongoza chaaaa!!! mpaka wanatia aibu. Kila siku tunataka kwenda nchi za wenzetu, mbona wenzetu sio issue kwa kungangania kusafirisafiri, wakisafiri wao ni kutalii na binafsi na analikizo yake, na pocket money yake, sio ya kuliangamiza taifa,

Anonymous said...

Na yeye mwenywe membe ni jipu, atawezaje kutoa kauli ya kumpongeza,si itakuwa unafiki, anono hapo juu

Anonymous said...

Mhe Membe angepumua kidogo na kuvuta pumzi asingejidhalilisha kiasi hichi. Wahenga walisema subira yaleta kheri. Hawakukosea hata kidogo.

Anonymous said...

kiburi na fedhuli ya membe si ya peke yake.maoni yake,kama ukiyachunguza sana yamepewa uzito na yanaungwa mkono na swahiba wake wa karibu,shemeji yake,mstaafu rais wa awamu ya nne.huyu ndiye anayethubutu kumpa jeuri hii,ufedhuli huu,bernard membe.ni chokochoko kamili tena imesukwa kweli kweli.anayoyaongea membe ni ya kipuuzi,hayana mashiko na yamejaa hasira ya kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais ndani ya kambi ya ccm membe alishika mkia kwenye mchujo wa tano bora kutafuta mbili bora pamoja na nguvu yote ya kikwete.kikwete alimuandaa membe kikamilifu na zilitumiwa kila aina ya mbinu, nyingi zikiwa chafu kupindukia.dawa iliyopo hapa ni muheshimiwa rais wetu,john pombe magufuli kuanza kuchukua hatua thabiti na za dhati KUANZA UCHUNGUZI WA MATUMIZI MABAYA YA OFISI NA RASLIMALI ZA TAIFA KWA UONGOZI WA JUU WA AWAMU YA NNE TANZANIA.MNANIELEWA SIJUI?.NASEMA HIVI, ALIYO NAYO MOYONI KIKWETE NDIYO HAYA ALIYOYAWAKILISHA MEMBE.KAMA MNA WASI WASI NA HILI BASI WAANDISHI MTAFUTENI MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE MUMHOJI KATIKA MSTALI ULE ULE ALIOHOJIWA MHE.BERNARD MEMBE.nawakilisha hoja hii kwENU.

Anonymous said...

WADAU MLIOANDIKA ANTI-MEMBE OPINIONS MUWE MAKINI KIDOGO. MEMBE NI MSOMI WA HAPA MAREKANI, KAMA WENGI WETU TUNAOCHANGIA HAPA. ALIKUWA WAZIRI KATIKA AWAMU YA NNE (MIAKA TISA). KUMBUKENI KUWA NI MEMBE NA JITIHADA ZA SERIKALI YA AWAMU YA NNE (YA RAIS MSTAAFU KIKWETE) NDIYO WALIWEZESHA KUISHAURI, KUIKARIBISHA NA KUIVUTIA SERIKALI YA MAREKANI KUTUPA MABILIONI AMBAYO YAMELIWEZESHA TAIFA LETU KUKAMILISHA MIRADI MINGI. SEKTA NYINGI ZA KIUCHUMI ZIMENUFAIKA NA PESA ZA MAREKANI, KUANZIA BARABARA KATIKA MIKOA MINGI (MILLENEUM FUNDS), UWEKEZAJI KATIKA ENERGY SEKTA (e.g.GAS), WATALII WA KIMAREKANI, N.K. WABONGO WENGI HAMJASAHAU UJIO WA MARAIS BUSH NA OBAMA NCHINI TANZANIA. FOLKS! DO YOU KNOW WHO WORKED BEHIND THE SCENE? HATA WACHINA WAMEONGEZA UWEKEZAJI KUTOKANA NA UHODARI WA SERIKALI YA AWAMU YA NNE NA DIPLOMASIA YA MEMBE, PERIOD. TUACHE USHABIKI USIO NA BUSARA NA TUWAPE CREDIT VIONGOZI WOTE WALIOPITA, INSTEAD OF TRASHING THEM. OF COURSE, THEY WERE NOT PERFECT, BUT THEY PLAYED A POSITIVE ROLE IN OUR LIVES. NAKUBALIANA NA MEMBE, KUWA HATUWEZI KUWA ISOLATIONISTS, AMA SIVYO TUTAKWAMA KUWAVUTIA INVESTORS. DR.TEMBA, KUMBUKA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI SEFUE AMEFANYA KAZI CHINI YA MARAIS MKAPA, KIKWETE, NA SASA DR. MAGUFULI. NINA UHAKIKA ATAKUBALIANA NA MAONI MENGI YA MEMBE, INGAWA HATAWEZA KUSEMA HIVYO HADHARANI. WADAU, NI KWELI RAIS WETU JPM AMEANZA KAZI VIZURI SANA, HIVYO BASI LAZIMA TUENDELEZE MAHUSIANO MEMA NA MATAIFA MENGINE. NI MUHIMU RAIS WETU AKAJITAMBULISHE UGHAIBUNI MAPEMA ILI KUENDELEZA JUHUDI ZILIZOFANYWA NA MARAIS MKAPA NA KIKWETE KUIWEKA TANZANIA JUU. NDUGU WABONGO, CRITISM IS AN INTERGRAL PART OF ANY DEMOCRACY, HIVYO BASI KUMKOSOA JPM KUNAONYESHA HOW MATURE OUR DEMOCRACY IS. D.J. LUKE, BAADHI YA SISI WANADMV NA WANADIASPORA MAREKANI HATUWEZI KUZISAHAU EFFORTS ZA MEMBE KATIKA DUAL CITIZENSHIP STRUGGLES ZETU.

Anonymous said...

Please Membe give me a break.Is better to be quiet If you don't have anything positive to say.Thank you Mr Membe.

Anonymous said...

Wewe unaesema membe ni msomi wa Marekani umesahau usemi unaosema kusoma sio kuelimika. Miongoni mwa watumishi wa umma waliotumbuliwa majipu na serikali ya maghufuli kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kulitumikia taifa ipasavyo wanaelimu zaidi ya membe tumejionea wenyewe jinsi gani mkuu wa takukuru alivyokuwa na elimu kuzidi umri wake lakini mwisho wa siku baada ya kuzuia rushwa kadhalisha rushwa zaidi nchini. Kumsifia kiongozi wa nchi fulani kuwa hodari wa kuomba misaada ni upuuzi mtupu. Jamani kwa tunaoishi huku nje hasa marekani mtoto akeshafika miaka 18 ni mtu wa kujitegemea hahitaji tena misada kutoka kwa mtu kama wakwenda college atakwenda college lakini tayari ameshajengeka katika mind set ya kujitegemea. Wakati mwengine mtoto wa miaka kumi na sita 16 tayari keshaanza kujitegemea. Sasa nchi yetu inamiaka mingapi bado tu tunajisifia mahodari wa kuomba ni aibu hiyo jamani.viongozi wetu wanapokuja huku kuomba misaada hawa wazungu wanawashangaa sana kwani mambo kama hayo hayapo katika system yao ya maisha kwani hata mtoto wa miaka mitano nyumba anaoishi ya wazee wake humsikii akiita our house isipokuwa atiita dad's house or mom's house. Sisi mungu katujaalia katika nchi zetu rasilimali za kutosha kama vile watu tena vijana ni wengi zaidi katika jamii yetu lakini viongozi wetu wameshindwa kuutumia utajiri huo wa nguvu za vijana kuiendeleza nchi matokeo wanakimbilia kuomba nje na hata hiyo misaada ikipatikana inaishia mifukuni mwa wakubwa. Licha ya rasilimali ya watu nchi kama Tanzania tuna kila Kitu cha thamani cha kututoa katika umaskini, dhahabu,almasi,tanzanite, very beautiful wildlife wonderland for tourism, don't forget mount Kilimanjaro if our leaders are smart and honest only mount Kilimanjaro could make Tanzania rich and very well known around the world. Usisahau sasa tuna gas,achana na mapato ya ndani yanayopatikana na bandari na kadhalika.sasa utajiri wote huo kwanini watanzania tuishi kwa kutegemea kuomba?kwa nini tusijetemee tuna ardhi ya kilimo inayoweza kudhalisha kila aina ya vyakula na matunda ati maaple tunaagiza kutoka nje? Sijafika lushoto lakini nasikia kuna baridi, isipokuwa nimefika arusha a,iringa,na mbeya hizo sehemu zinauwezo wa kuzalisha maaple ya kutosha kabisa hata kusafirisha kibiashara kutokana na hali ya hewa yake. Sasa kitu gani kinachomfanya mtu wa miaka arubaini mpaka hamsini kama umri wa nchi yetu kuishi kwa kuomba omba? Ukimuona mtu wa umri huu anapita akiomba omba basi kuna mambo kadhaa yamemtokezea katika maisha yake. La kwanza ugonjwa wa akili. Pili kutokuwa na aibu na kujijengea mazoea ya kuomba omba na kujiondeshea hali ya kuishi kwa kujitegemea. Tatu uvivu wa mwili na akili. Naona wakati umefika watanzania kusema enough is enough wakati wa kuwajibika umefika kwa manufaa ya Taifa si maneno tu bali kwa vitendo.

Anonymous said...

Eti Membe msomi wa Marekani!!haa haaaa haaaa Sooo, wasomi wa Afrika hawana akili sio. Pleeease haaa haaa chaiiiii

Anonymous said...

Kwa nini asilimia kubwa ya walioachishwa na kufukuzishwa kazi ni wasomi waliopata elimu zao za juu ughaibuni? Yaelekea locally educated professionals wanapendelewa kidogo, hali ambayo inaweza kusababisha "brain drain phenomenon" kama ile ya miaka ya 70s na 80s enzi za "socialism".

Anonymous said...

Kwanini watumishi wa kawaida tu serekalini walikuwa wanasafiri business class? Tanzania ilikuwa na hela gani kusafirisha hao watu business class?