Ni juzi tu naibu waziri wa mambo ya ndani muandisi Mhe.Hamad Masauni aliiagiza Idara ya Uhamiaji kusaka na kuwakamata raia wageni wote wanaochukua ajira zinazoweza kufanywa na wataanzania, wito huo tayari umeshaitikiwa na idara ya uhamiaji mkoa Dar-es-salaam kama alivyosema Afisa Uhamiaji mkoa Bw.John Msumule kuwa watawasaka wahamiaji wanao chukua ajira za watanzania na kuwafikisha mahakamani.
Mashaka ya ubaguzi katika kamata kamata hiyo! inawezekana zoezi hilo likafanyika kwa
ubaguzi bila makusudi,na wakakamatwa mfano raia wa Somali na wahabeshi wanauza milungi,warundi na wanyarwanda ambao ni wakimbizi, namakundi mengine ambao ndio
vinara wanaoongoza kwa kunyakua ajira zinazowezwa kufanywa na watanzania wakaachwa.
Mfano katika maeneo ya Kariakoo kuna wachina wanauza maduka na wanamiliki maduka tunajiuliza hivi kweli vibali vya uwekezaji vinatolewa ovyo mpaka
kwa wachina kuwekeza katika maduka?!
WAZUNGU NAO WAMO ! kuna raia wengi wa kizungu wameingia hapa kwa viza za kutalii na sasa wanafanya kazi mpaka za upishi na kutembeza watalii ! sasa inashangaza hii nchi kweli Shamba la Bibi ?
KUNA MADANGULO yenye machangudoa kutoka Asia nayo yasakwe pia
Kuna walinzi makolokoloni raia wa kigeni nao wanavibali vya kuishi na kupata ajira hapa nchini ?!
Leo tunao hapa nchini Wachungaji katika makanisa ! wachungaji hao wengi wao toka Nigeria na makanisa yao yameibuka kama uyoga na kupata vibali vya kuendesha shughuli zao Tanzania!
Wanenguaji na Marapa katika bendi za muziki nao pia kutoka nje ya nchi! hivi kunengua nako kuwashinde watanzania ?
TUNAIOMBA IDARA YA UHAMIAJI IFUTE NA KUVIHAKIKI VIBALI VYOTE VYA WAGENI
Zoezi hili lazima liwashikirikishe wananchi na serikali za mitaa
Hapa Kazi TU
4 comments:
Wasiwaonee
Mbona kuna wabongo kibao ughaibuni
Wamejiripuwa wakimbizi toka Somalia Na inchi nyingine
Cha msingi
Kama hawaibi wanafanya kazi zao it's ok
Watanzania tuwe waugwana kidogo . Watanzania wengi wapo kola nchi duniani walio jilipua na wasio . Wote wanatafuta maisha . Kama hao wachina wachapa kazi hawana uwizi hawaingili siasa mie naona Poa tu . It's part of life everybody have to try to survive. We shouldn't make a big issue . Tukumbuke kuna Ndugu na jamaa zetu ughaibuni hawana vibali vya kuishi. Tusisahau South Africa walivotufanyia tuka chukia sana. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu .............
Motor City umeongea vizuri kweeeli.
Mchina mchana muuza ugali barabarani usiku ni agenti wa kusafirisha meno ya tembo.uchunguzi uliofanywa na mashirika ya kuzuia ujangiri duniani inaonesha baadhi ya raia wa kigeni hasa wachina wanahusika na uangamizaji wa tembo na faru Africa.
Post a Comment