(IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO MAMBO YA NDANI YA NCHI)
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akisalimiana na Naibu Kamishna wa uhamiaji Haji Hamza wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Uhamiaji Zanzibar zilizopo katika eneo la Kilimanim, kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu
Naibu Waziri wa Mmambo ya Ndani ya Nnchi Hamad Masauni akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Kamishina Mkuu wa Uhamiaji Zanzibar alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji katika ofisi hizo zilizoko Kilimani Zanznibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Visiwani Zanzniabr waliokuwa wakisubiri huduma katika ofisi za Uhamijia alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji zilizoko Kilimani Zanznibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akisikiliza maelezo ya hatua za maombi ya hati za kusariria kutoka kwa afisa wa udhibiti wa hati za kusafiria katika ofisi za Uhamiaji Zanzibar alipofanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kujione shughuli mbalimbali za kiutendaji
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni (kushoto) akiongozana na Kamishna wa Uhamijai Zanznibar , Johari Sururu (Kulia) kuelekea katika chumba cha kuhiofadhi kumbumbuku za waombaji hati za kusafiria. Naibu huyo alitembelea ofisi hizo kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji katika ofisi hizo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akikagua jarada lenye kuonyesha kumbukumbu za waombaji wa hati za kusafiria kutoka katika familia yake, aliyesimama ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzniabr Johari Sururu akifatiwa na Naibu Kamishna wa Utawala na fedha. Masauni alifanya ziara hiyo ya kikazi kwa ajili ya kujionea shighuli mbalimbali za kiutendaji.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akizungumza na watendaji wakuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar alikofanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji. Waziri huyo ametoa onyo kwa maafisa wote wanaotumia zoezi la kukamata wahamiaji haramu kinyume na agizo la serikali kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amewataka Maafisa Uhamiaji kutotumia nafasi ya kukamata wahamiaji haramu kinyume na matakwa ya Serikali pamoja na Sheria za nchi.
Hayo aliyazungumza katika Ofisi kuu ya Uhamijai Zanzibar iliyopo eneo la Kilimani alipofanya ziara yake ya kikazi ili kujionea shughuli za utendaji wa ofisi hiyo.
Waziri huyo amesema kuwa Serikali chini ya Idara ya Uhamiaji itapambana na wahamiaji waliopo nchini bila vibali ama kufuata kanuni na sheria zinazoruhusu ukaazi wao na si vinginevyo. Hivyo wageni wote wenye vibali vinavyowaruhusu kuwepo nchini hawato bugudhiwa kwa namna yoyote ile, na yeyoye atakae bainika kunyanyasa wageni hao wenye vibali atachukuliwa hatua za kinidhamu.
“Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani kote tunapenda wageni, tunajua kwamba watalii, na wawekezaji waliopo nchini wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa taifa letu, hivyo hatuwezi kuwafukuza ama kuwanyanyasa kama wako nchini kihalali” alisema Bw. Masauni.
Aidha amewataka maafisa wa uhamijia kuto tumia zoezi hilo la kubaini wakaazi haramu kwa manufaa yao na yeyote atakae bainika kutumia zoezi hilo kinyume na agizo la serikali atashughulikiwa kwani serikali haijapanga kuonea wala kunyanyasa mtu yeyote yule.
Naibu huyo aliongeza kuwa sheria zilizopo nchini ni kwa ajili ya manufaa ya nchi hivyo ni lazima kila mtu aziheshimu na kuwa Serikali haina lengo la kutumia sheria hizo kukandamiza wageni.
Pamoja na hayo Masauni alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kutatua kero za wananchi, hivyo Idara ya Uhamiji itaendelea kuwatumikia wananchi kwa weledi wa hali ya juu na kuhakikisha kero zote za awali zinatatuliwa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake