Haruna Niyozima wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazoezi na klabu yake
Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima ambaye mkataba wake na klabu hiyo ulivunjwa kutokana na makosa ya kinidhamu ya nahodha huyo wa Rwanda, leo ameanza rasmi mazoezi na kikosi cha wakali hao wa Jangwani kwenye uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Wiki iliyopita Niyonzima aliuomba radhi uongozi, wachezaji wenzake, wanachama na mashabiki wa Yanga kutokana na yeye kuchelewa kurejea kikosini mara baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa na kudai kulikuwa na mawasiliano mabovu kati yake na uongozi wa klabu hiyo.
Niyonzima amesema anashuru kurejea tena kwenye kikosi cha Yanga na kuungana na wachezaji wenzake na kusisitiza hata wakati yuko nje ya timu bado alikuwa akiwasiliana na baadhi ya wachezaji na kuwasisitiza kukomaa ili watwae ndoo tena msimu huu.
“Nashukuru kwa nafasi nyingine, naipenda sana Yanga nafurahi kuungana na wenzangu tena. Hata kipindi niliposimamishwa niliendelea kuwasiliana na wenzangu kuwatia moyo na kuwakumbusha kuwa msimu huu tubebe ubingwa pia kwani hiyo ndio heshima yetu pekee na kudhihirisha ubora wetu”.
Uongozi wa Yanga ulitangaza kuvunja mkataba na nyota huyo na kudai kulipwa mamilioni ya pesa kama fidia ya mkataba wake unaomalizika mwaka 2017. Lakini wameshayajenga na tayari mnyarwanda huyo amerejea kikosi kuungana na wachezaji wengine wa kikosi hicho.CREDIT:Shaffih Dauda.
No comments:
Post a Comment