Friday, January 22, 2016

Rais Magufuli Avaa Sare za Jeshi Akiwa Arusha

Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine kesho Januari 23, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya Sanawali, Tekniko, Ngarenalo, Mbauda, Majengo na Kisongo.
Wananchi waliojitokeza kumlaki rais Magufuli.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.

6 comments:

  1. Mzee sare zimemchukua hasa ila licha ya watanzania tunakutaka uwe kamanda wa maendeleo zaidi.

    ReplyDelete
  2. Kavaa sare zimempendeza sana. Naamini alipitia JKT enzi ile baada ya elimu ya form four. Kwa hiyo yeye ni mkuu haswaa wa Majeshi. Tumheshimu na kuuheshimu uongazi wake na kuzingatia nidhamu katika maisha. Tuchunge muda, time, amani, na upendo.

    ReplyDelete
  3. amri jeshi mkuu siyo mwanajeshi. Ingemake sense kama hizi uniform angevaa JK vinginevyo Magufuli anajichora kama Bush alivyovaa air force uniform kwenye mission accomplished.

    ReplyDelete
  4. Acha chuki ndugu huyo ndio jemedari wetu mkuu Mungu akulinde ameen

    ReplyDelete
  5. VICKY ROSE, JUST FOR YOUR INFO, JPM ALIKWENDA JKT BAADA YA KUHITIMU A-LEVEL i.e. FORM SIX PALE MKWAWA HIGH SCHOOL. ENZI ZILE JKT ILIKUWA NI COMPULSORY IMMEDIATELY AFTER FORM SIX OR KAMA UMEHITIMU CERTIFICATE FULANI BEYOND FORM FOUR. KWA MDAU WA 12:46 PM, NADHANI RAIS JPM AMEVAA UNIFORM IN SOLIDARITY WITH OUR SOLDIERS SACRIFICE TO DEFEND OUR NATION, AND ALSO KUONYESHA HESHIMA KWA WANAJESHI WETU. BINAFSI SIONI KAMA ANATAKA KU-PROVE ANYTHING. NI SAWA KAMA WEWE UKITEMBELEA SCIENTIFIC RESEARCH LABS, WATAKUVALISHA WHITE COATS, HAIR-NETS, SAFETY GOGGLES, N.K.

    ReplyDelete
  6. That uniform represents leadership discipline excellence and thats what Magufuli represents. Very proud to call him my Commander In Chief

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake