Thursday, January 14, 2016

RC MAHIZA ATEMBELEA BANDARI YA TANGA AKUTANA NA WAFANYAKAZI

,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza akizungumza nawatumishi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) mkoani Tanga jana wakati alipofanya ziara ya kuangalia utendaji wao na changamoto 
zinazowakabili. 
Picha zote kwa Hisani ya Tanga Raha Blog.
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi akizungumzawakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga alipoifanya kwenye Mamlaka ya Bandari (TPA) Tangaya kutembelea Bandari hiyo na kuangalia utendaji wao na changamoto zinazowakabili.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari (TPA) MkoaniTanga,Henry Arika akizungumza wakati wa wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga aliyoifanya ya kutembelea Bandari hiyo na kuangalia utendaji wao na changamoto zinazowakabili.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mustapha Selebosiakiwasalimia wafanyakazi wa mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga (TPA) wakati wa wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga aliyoifanya ya kutembelea Bandari hiyo na kuangalia utendaji wao na changamoto zinazowakabili.
wa pili kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Mamlaka yaBandari (TPA) Mkoani Tanga,Henry Arika akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza wa kwanza kushoto wakati alipofanya ya kutembelea bandari hiyo na kuangalia namna ya utendaji wao na changamoto zinazowakabili.
watumishi wa Mamlaka ya Bandari mkoaniTanga(TPA) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza wakati alipofanya ziara ya kutembelea bandari hiyo na kuangalia namna yautendaji wao na changamoto zinazowakabili
 watumishi wa Mamlaka ya Bandari mkoaniTanga(TPA) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza wakati alipofanya ziara ya kutembelea bandari hiyo na kuangalia namna yautendaji wao na changamoto zinazowakabili
kushoto ni Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari (TPA)Mkoani Tanga,Henry Arika akimuonyesha jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza wa kwanza kushoto wakati alipofanya ya
kutembelea bandari hiyo na kuangalia namna ya utendaji wao na changamoto zinazowakabili.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Bandari ya Tanga(TPA),Moni Jarufu Msemo akitoa neon la shukrani mara baada ya mkuu wa mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza kumaliza kuzungumza na
wafanyakazi.

NA MWANDISHI WETU,TANGA.
IMEELEZWA kuwa agizo la Rais John Magufuli kusitisha safari za nje kwa watendaji wa serikali nchini zimesababisha Bandari ya Tanga kufanyakazi chini ya kiwango na kulazimika kukodi vifaa kwa gharama kubwa nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa bandari ya Tanga,Henry Arika wakati mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alipofanya ziara ya siku mmoja kukagua shughuli zinazofanywa na bandari hiyo.

Alisema kuwa hatua hiyo ya kusitishwa kwa safari mpaka vibali imechangia bandari hiyo kupata hasara na kulazimika kukodi Tug ya kupakuwa mizigo kutoka nangani kwenye meli hadi katika pwani ya bandari hiyo.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa japo agizo hilo linafaida kwa serikali lakini tunamuomba Mheshimiwa Rais angalie upya agizo hilo kwani kuna baadhi ya taasisi zinazojiendesha kibiashara zinaathirika na utendaji wake wa kila siku kushuka”alibainisha Kaimu Meneja huyo.

Aliiomba serikali kuangalia namna bora ya kutenganisha taasisi hizo katika utoaji wa vibali kwani kwa hili limesababisha kushindwa kupelekaTug meli ya kukokotea vyombo vya majini yao kwa ajili ya ukarabati nchini Kenya.

“Tagi tuliyonayo katika bandari ya Tanga ni mmoja pekee na manahoza waliisimamisha kufanyakazi toka mwezi Novemba mwaka jana hivyo tumelazimika kukodi Tug kutoka mjini Mombasa ili kurahisisha utoaji wa mizigo”alisema Arika.

Ambapo aliongeza kuwa hali hiyo situ inakwamisha utendaji kazi bali inachangia hasara kwa Mamlaka kwani hulazimika kutumia gharama kubwa kwaajili ya uwendeshaji kifaa cha kukodisha.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa uwamuzi wa Rais ni kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana kwa haraka na kwa kutumia raslimali kwa uwangalifu.

Alisema kuwa sambamba na hilo ilikuweza kuongeza ufanisi katika bandari ameahidi kuunda tume itakayokuwa ikishughulika na kutatua kero mbalimbali zinazoikabili bandari hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi .

No comments: