ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 23, 2016

SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA UZALISHAJI NA MATUMIZI ENDELEVU YA RASILIMALI

 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George Pangawe akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu wananchi kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji  nchini pale wanapotaka kuendeleza ardhi kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta na kulia ni Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara

 Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari  Jijini Dar es Salaam kulia niMsaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George Pangawe na kushoto ni 
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta



Hassan Silayo-MAELEZO 
 Serikali kuendelea kutoa elimu ya Uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali kwa wananchi ili waweze kunufaika na rasilimali zote zilizopo katika maeneo yao kote nchini. 
 Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Bw.Carlos Mbuta wakati wa mkutano na vyombo vya Habari ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuelimisha umma kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali ikiwemo ardhi. 
Akifafanua Mbuta amesema kuwa Elimu hiyo itawasaidia wananchi kungamua na kufanya maamuzi sahihi pale wanapotaka kutumia rasilimali zilizopo katika kujiletea maendeleo.
 ’Elimu ya mazingira imejumuishwa katika mitaala ya shule zetu hapa nchini ili kujenga uelewa kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali alisisitiza Mbuta Akizungumzia faida za Elimu ya Mazingira kutlowa mashuleni mbuta alibainisha kuwa itasaidia kujenga kizazi chenye uelewa na uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo kwa kuzingatia sheria na kanuni.
 Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. George Pangawe alitoa wito kwa wananchi kufuata taratibu zote za kisheria pale wanapotaka kuendeleza Kipande chochote cha ardhi. 
 Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara yake inasimamia matumizi sahihi ya uendelezaji wa ardhi na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusimamia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ya ardhi. 
 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mazingira pamoja na Halmashuri zote nchini zimekuwa zikisisitiza kuhusu elimu ya uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali ili ziweze kuwanufaisha wananchi.

No comments: