Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto
Dkt.Hamisi Kigwangalla (kulia)akitembelea jana
Makazi ya Wazee walioathirika na
ugonjwa wa ukoma yaliyopo kijiji cha Nunge
eneo la Kigamboni jijini Dar
es Salaam.mwenye shati la batiki Mkuu wa
Makazi hayo Moses Gunza.
Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla
akimsikiliza mmoja wa wazee aliyejulikana kwa jina la Salum Ubwabwa wakati alipotembelea jana Makazi ya Wazee walioathirika na ugonjwa wa ukoma yaliyopo
kijiji cha Nunge eneo la Kigamboni jijini Dar es
Salaam.Mzee huyo ambaye alimpatia historia ya eneo hilo, ambalo sasa
limevamiwa na baadhi ya watu.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
Dkt.Hamisi Kigwangalla akiangalia mazingira ya makazi hayo.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
Dkt.Hamisi Kigwangalla akielekea moja ya
maliwatoni katika Makazi ya Wazee walioathirika na ugonjwa wa ukoma yaliyopo
kijiji cha Nunge eneo la Kigamboni jijini Dar es
Salaam, wakati alipofanya ziara ya kutembelea makazi hayo jana ili kuangalia mazingira
halisi.
(Picha na Catherine Sungura-WAMJW)
Serikali imewataka wananchi waliovamia eneo la kambi ya kuwalea wazee walioathirika na ugonjwa
wa ukoma yaliyopo Nunge Kigamboni, kusitisha mara moja ujenzi wa nyumba
zao ama kubomoa wenyewe ndani ya siku 21 kabla hatua ya kubolewa
haijachukuliwa.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii wazee na
watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla, wakati alipowatembelea jana na kukuta
idadi kubwa ya nyumba za wananchi mbalimbali zilizojengwa ndani ya ardhi
ya makazi hayo ya wazee.
Kufuatia
hali hiyo ,Dkt. Kigangwalla amemuagiza Mkuu wa kambi hiyo ya wazee
Moses Gunza kutoa notisi ya kusitisha ujenzi na ikiwezekana wananchi hao
wabomoe wenyewe nyumba zao kabla Serikali haijafika kuwabomolea.
“Hivi
kweli watu wanaona kabisa makaburi haya watu wamezikwa hapa tangu enzi
za mjerumani halafu wananunua na kujenga haiwezekani kuchezewa kiasi
hiki watu wafike sehemu waiheshimu Serikali na kufuata sheria za
nchi,”alisema Dkt. Kigwangalla.
Dkt.
Kigwangalla eneo hilo la Nunge limewekwa kwa ajili ya kulea na
kuhudumia watu waliokuwa wakiuugua ugonjwa wa ukoma sasa iweje ajitokeze
mjukuu wa kati ya wazee hao awauzie watu na ardhi hiyo huku akidai kuwa
eneo hilo ni mali yake iliyotokana na urithi wa babu yake jambo ambalo
sio kweli.
“Ninatoa
siku 21 watu hawa wote waliojenga katika makazi haya ya wazee kusitisha
mara moja ujenzi wa nyumba zao au kubomoa na hiyo mtu anayedai eneo
hili ni lake akija hapa akatoa maagizo yake mnipe taarifa nitamuweka
ndani.,”alisema Dkt. Kigwangalla.
Akipokea
akigizo hilo mkuu wa kambi hiyo Moses Gunze alisema wananchi hao
walikwisha pewa notisi tangu mwaka jana 2015 na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ya kuwataka wananchi waliopo eneo lote la Nunge kusitisha zoezi
la kuendelea kujenga nyumba zao agizo ambalo halikutekelezwa kutokana
na muingiliano wa kisiasa.
“Hawa
watu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alishatoa stop order ya kuwataka
wasiindelee na ujenzi wowote hapa lakini baadaye wananchi hawa
wakajipanga wakaenda Bungeni Dodoma na baadaye aliyekuwa Waziri wa afya
Dkt. Seif Rashid akatoa barua akasimamisha zuio matokeo yake watu
wakaendelea kujenga tena, ’’alisema Moses.
Kwa
upande wake mzee Salumu Ubwabwa ambayea ameathirika na ukoma
anayelelewa katika kituo hicho amebainisha kuwa kuna anayejulikana kwa
jina la Bahari Seifu anayewauzia watu viwanja akidai kuwa eneo hilo la
Nunge ni lake amerithi kutoka kwa babu yake Mohamedi Sheweji.
Mzee
Ubwabwa amebainisha kuwa yeye amefika katika makambi hayo tangu mwaka
1984 baada ya kuugua ukoma kutokana na miaka hiyo watu wa ukoma kutengwa
mjerumani akawajengea jumba la mabati na kuwahifadhi huko Kigamboni ili
wasiweze kuvuka kwenda ng’ambo kwani wangeweza kusababisha maambukizi.
Alisema
mwaka 1974 Rais wa kwanza Hayati Julius Nyerere aliwajengea nyumba hizo
na Serikali ya Tanzania ikaendelea kuwatunza hadi sasa.
Mzee
Ubwabwa alisema katika makambi hayo alikuwepo na mzee Mohamedi Sheweji
ambaye naye alikuwa mgonjwa wa ukoma alihifadhiwa kwenye makambi hayo
hivyo anashangaa kuona Bahari Seif akijitokeza hivi sasa na kuanza
kuuzia watu viwanja kwa madi kuwa ardhi ya Nunge ni uridhi wa babu yake
wakati si kweli.
No comments:
Post a Comment