Monday, January 11, 2016

TASWIRA YA MHE.BALOZI WILSON M. MASILINGI AKUTANA WANADIASPORA WEEKEND NEW YORK CITY.


Mhe.Balozi Wilson M. Masilingi Balozi wa Tanzania Marekani alikutana na Watanzania wenye Taaluma, Biashara na Company binafsi, Balozi aliitisha mkutano huo uliofanyika ndani ya Ukumbi wa mikutano wa Tanzania Mission New York City. Balozi aliongea kwa ufafanuzi juu ya jinsi gani anataka kushirikiana na wale wote wenye nia ya kufanya mambo ya kimaendeleo kwa ajili ya nchi yao ya Tanzania. Balozi alisisitiza nakusema Watanzania wote wenye nia hiyo wajitokeza na kuwasiliana nae, kwani rais wa awamu ya tano ametoa fulsa ya Watanzania wote wenye Taaluma, Elimu na wenye mipango ya kuwekeza Tanzania wajitokeze na kuwasiliana nae ili kufanikisha yale yote yanayo weza kuiletea nchi ya Tanzania maendeleo. Mhe. Aliongea hayo yote kwa msisitizo na kurudia mara kwa mara kauli mbiu ya rais wa awamu ya tano ya #Hapa Kazi tu#. Mkutano huu uliandaliwa na Tanzania Mission New York City.

Wanadiaspora wakimsikiliza Balozi ndani ya ukumbi wa mikutano wa Tanzania House New York City. Kwa Picha zaidi jitiririshe chini kwa kubonyeza soma zaidi.


Dr. Temba mwenye company ya T.E.S akichangia hoja mbele ya Mhe. Balozi Masilingi , Dr. Temba ni Engineer na Designer wa Smoke House na Air Pollution System machine.

Bwana Waluya akichangia jambo na yeye juu ya ujuzi alionao na jinsi alivyo kuwa na mipango ya kuwekeza Tanzania.

Bwana Mushumbuzi Mkatalasi aliye bobea mwenye mipango ya kwenda kuitumia taaluma yake hiyo Tanzania.

Mhe.Balozi Masilingi akiagana na Watanzania baada ya mkutano kwisha Mhe. Balozi aliondoka na kurudi Washington. DC kuendelea na majukumu mengine ya kikazi.

Kilicho nivutia katika mkutano huo ni hakukuwa na chakula zaidi ya maji madogo, juice soda na cookies habari ndiyo hiyo kama ukula nyumbani kwako hapa kazi tu.
Picha ya pamoja na Mhe. Balozi Masilingi na Watanzania ndani ya Tanzania House.

2 comments:

Anonymous said...

Sasa kazi tu. Waje kuwekeza nyumbani. Kumbe pesa yote ilikuwa imebanwa nje.

Anonymous said...



Moja ya mikutano yenye Tija ,aksante Balozi.

Sylvester