Wachezaji wa Toto Africans (Jezi za Njano) wakisalimiana na wachezaji wa Pamba, kabla ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza hii leo. Katika Mchezo huo Toto wamewatupa nje ya michuano hiyo majirani zao Pamba kwa jumla ya magori 4-1.
Magoli ya Toto yamefungwa na Miraji Athuman Madenga aliefunga magoli mawili, Eddo Christopher pamoja na Waziri Junior Shentembo huku bao la Pamba likifungwa na James Sungura.
Kwa matokeo hayo, Pamba wametupwa nje ya Michuano hiyo na Toto wameweza kusonga mbele na kutinga hatua ya 16 bora.
Kamisaa wa mchezo akiwa katika picha ya pamoja na Waamuzi pamoja na Makeptaini wa timu za Pamba na Toto.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mwanza (Katikati) akiwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia mchezo kati ya Toto na Pamba
Shambulizi langoni mwa Timu ya Pamba
Wachezaji wa Toto Africans wakishangilia ushindi wao dhidi ya timu ya Pamba katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Bado kuna mwitikio mdogo wa mashabiki wa soka kufika uwanjani Jijini Mwanza. Hapo ni jukwaa kuu.
Wanahabari
Kushoto ni Gervas Mbaya ambae ni Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya Pamba akiteta jambo na bwana Cathbert ambae ni Msemaji wa Timu ya Toto Africans. Katikati ni Mwanahabari Moses Methew.
Kushoto ni Hashim Kibode ambae ni Team Manager wa Timu ya Pamba, katikati ni Kocha Msaidizi wa Timu hiyo Yangoo Mamboleo na Kulia ni Afisa Habari na Mahusiano Gervas Mbaya wakiteta jambo baada ya kutolewa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho na Timu ya Toto kwa kutundikwa bao 4-1.
Dominik Glawogger ambae ni Kocha Mkuu wa Timu ya Toto (Katikati) akizungumza na wanahabari baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya timu ya Pamba.
Mdau wa Michezo akiwa katika mahojiano
Kutoka Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Mimi ni GB Pazzo, Mzee wa Ekotitee wa Binagi Media Group.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake