Monday, January 4, 2016

WADAU WA MAJI WATEMBELEA MAENEO YA NJIA ZA ASILI ZA MITO INAYOMWAGA MAJI

U6
Wataalum kutoka Wizara ya Nishati na Madini , Wizara ya kilimo ,uvuvi na mifugo, Wizara ya maji na umwagiliaji pamoja na watalaam kutoka bonge la mto Rufiji wakipita eneo ambalo kumejengwa tuta ili kuzua njia ya asili ya moja ya mito inayomwaga maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji kwa nia ya kupisha ujenzi wa mfereji wa maji yatakayotumika katika kilimo cha umwagiliaji, jambo ambalo limedaiwa kuwa huathiri mazingira na utiririshaji wa maji katika mabwawa.
Wadau wa maji waliotembelea maeneo ya mito na kugundua baadhi ya njia za asili za mito inayomwaga maji yake kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme imezibwa.
kitendo hicho kinadaiwa kuathiri utiririshaji wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.
pia wadau hao wameshauri taasisi zote ikiwemo wizara ya nishati na madini,wizara ya kilimo , mifugo na uvuvi, wizara ya maji na umwagiliaji pamoja na bonde la mto rifiji zinazotumia rasilimali maji katika shughuli zake kushirikiana ili kumaliza tatizo la kukauka na kupungua kwa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.
U1
Cable wire za Umeme zikipitishwa katika moja ya njia zililizopo chini ya mwamba wa mlima( tannel) ambapo ndipo zilizopo mashine za kuzalisha umeme wa maji na shughuli zote za uzalishaji.

U2 U3
Mashine za kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, kidato na Mtera vinanyonekana ambapo shughuli zote za uzalisha wa umeme wa maji na mashine hizo ziko chini ya mwamba wa mlima uliotombelea .
U4
Sehemu iliyochepushwa maji kitaalamu kutoka katika moja ya mito inayomwaga maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ili maji hayo yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji.
U5
Tuta lilijengwa katika njia asili ya mto ili kupisha ujenzi wa mfereji wa maji yatakayotumika katika kilimo cha umwagiliaji, jambo ambalo limedaiwa kuwa huathiri mazingira na utiririshaji wa maji katika mabwawa.

No comments: