ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 28, 2016

WAKABIDHIWA JENGO LA MAFUNZO NA MADAWATI KILOMBERO

 Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi  jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa  5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
 Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero.
Mke wa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Louise Bainbridge akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilombero, Muungano, Kantui, Ujirani, Lyahira na Mapinduzi (hapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati  jana, Kilombero. Katiakti ni Meneja Mkuu wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mark Roe-Scott na kulia ni meneja utawala wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Allawi Mdee.

No comments: