Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Maniza Zaman alipokuja Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho wake kwa Mhe. Waziri Mahiga.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Bi. Zaman (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bi. Mindi Kasiga, Bi. Eva Ng'itu, Afisa Mambo ya Nje na Katibu wa Waziri, Bw. Thobias Makoba
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Bi. Maniza Zaman. Picha na Reginald Philip
No comments:
Post a Comment