
Balozi
Pierre Mutemba (katikati) akiimba wimbo wa Taifa.Na Maria Inviolata
Balozi
mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo nchini Tanzania
(DRC) Pierre Mutamba amewataka Wakongomani waishio nchini Tanzania
kuwa na umoja na kufanyakazi kwa bidii ili waweze kujenga nchi yao,
amesema hayo wakati Balozi huyo akianza kazi rasmi, leo katika ofisi
za Ubalozi huo zilizopo Upanga jijini Dar es salaam.
Balozi
Mutamba amewaambia wanajumuia hao kuwa falsafa yake ni “Ni hapa kazi tu”
inayofuata nyayo za Kauli Mbiu ya Rais John Pombe Magufuri wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi
Mutamba alitoa Bendera za Taifa lake kwa kila Kiongozi wa jumuia ya
Wakongomani waishio hapa nchini ikiwa ni ishara ya Uzalendo wa
Taifa lao, Balozi huyo alisema kuwa Bendera ni Nembo ya Nchi, kwa
hiyo ni jukumu la kila Mkongomani kuijenga nchi yake.
Wakongomani
waishio hapa nchini walimundalia Balozi Mutamba hafra fupi ya
kumkaribisha kufanya kazi hapa nchini, hafra hiyo ilifanyika katika
ofisi za Ubalozini huo. Viongozi wa jumuia mbalimbali za Wakongomani hao
wamesifu uteuzi wa Rais Joseph Kabila wa kumteua
Balozi Mutamba hapa
nchini, kwani uwakilishi wake umewapa matumaini, kwa
jinsi Balozi huyo alivyochukua hatua ya haraka kufungua milango kwa
Wakongo wote waishio hapa nchini ubalozini hapo kushirikiana naye kudumisha
uhusiano wa nchi hiyo na Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii.
Naye
Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (BCI) waishio hapa nchini Mukendi Kabobu amehaidi kuwa wafanyabiashara wa
chama hicho watampa ushirikiano mkubwa Balozi huyo kuondoa kero zote zilizokuwa
zikikwamisha shughuli zao. Rais wa chama cha hicho cha
wafanyabiashara, amesema kuwa chama hicho kinafanya kazi pamoja na
wafanyabiashara wa Tanzania na wengine wakiwa wanachama wa chama hicho.
Kabobu
amesifu utendaji wa Rais John Magufuri kwa kurekebisha mambo mengi kwa kipindi
kifupi cha uongozi wake. Mwenyekiti wa wazee wa Kikongomani hapa nchini
amemfananisha Balozi Pierre Mutamba na ‘Kichwa kizuri cha mashua’
ambaye atawavusha salama’ kwani Balozi huyo amekuja na falsafa ya kuwaunganisha
pamoja Wakongo wote.
No comments:
Post a Comment