Dk Kalemani alitoa rai hiyo juzi katika mkutano mkuu wa kwanza wa Numet, akisema njia pekee ya kumaliza matatizo ya wafanyakazi ni kufichua unyanyasaji unaofanywa na waajiri wageni.
“Shirikianeni na vyombo vingine vya uchunguzi kufuatilia maovu yanayofanywa migodini na wawekezaji, wajibu wenu ni kuishauri Serikali na kutupatia takwimu sahihi. Tutahakikisha tunazifanyia kazi taarifa mtakazotupatia.
“Undeni bodi itakayokisimamia chama, tasnia hii ina uwezo wa kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na |Taifa. Mkipata matatizo tushirikisheni tutakuwa bega kwa bega kuyapatia ufumbuzi,” alisema Dk Kalemani katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Albert Machumu alisema walisajili wanachama 3,413 kwa miaka mitatu, lakini kwa sasa wapo 1,857 baada ya wengine kuachishwa kazi kutokana na sababu mbalimbali.
Katika mkutano huo, chama hicho kilitoa tamko la kujiunga na kushirikiana na vyama vingine kuunda muungano wa vyama vya wafanyakazi mbali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) .
No comments:
Post a Comment