Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipokelewa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ilala, SACP Lucas Mkondya, alipofika kufunga kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
|
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu (kulia), akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, mara baada ya Katibu Mkuu huyo kumaliza
kutoa hotuba ya kufunga Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo
uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,
jijini Dar es Salaam.
|
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza wakati wa kufunga
kikao kazi cha Maafisa Maandamizi wa Jeshi
la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,
jijini Dar es Salaam. Wapili kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu.
|
|
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu, akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wakati
wa kufungwa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa hao uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wanne kushoto waliokaa), Mkuu
wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (kushoto kwa Katibu Mkuu) wakiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, mara baada ya kufungwa
Mkutano wao wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
No comments:
Post a Comment