ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 21, 2016

Lady In Red 2016 After Party ndani ya Regency Park hotel muda huu

Tayari designers wote pamoja na wadau wengine mbalimbali wa mitindo wanaendelea kujumuika ndani ya Regency Park Hotel ambapo kuna tukio moja tu la kukutana na kufurahia kwa pamoja baada ya show mbili za Lady In Red 2016 zilizofanyika Tanzania Januari 31 na ile iliyofanyika London, Februari 13 mwaka huu.

Mwandaaji wa Lady In Red, Mama wa Mitindo, Asya Idarous Khamsin anabainisha kuwa, ndani ya Party hii leo ni maalum kuwashukuru wale wote waliofanikisha pamoja na kuwatunukia vyeti (Certificate) za Shukrani.

…Hakuna kiingilio kila mtu anakaribishwa pia kuna min fashion show!!!
Mama wa Mitindo Asya Idarous Khamsin akiwa pamoja na baadhi ya Modelz 

Mama wa Mitindo Asya Idarous akiwa na moja ya vazi lake usiku huu..
Ankal Michuzi wa Michuziblog ambaye ni mgeni rasmi usiku huu akipata picha ya ukumbusho na Mama wa Mitindo Asya Idarous Khamsin…
Modelz katika ubora wake… (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog)

No comments: