Mbunge wa Segerea, Bonna Kaluwa amejenga madarasa matano katika Shule ya Msingi Kinyerezi Jica, ikiwa ni mkakati wake wa kukabiliana na upungufu wa madarasa jimboni humo.
Kaluwa amesema baada ya Rais John Magufuli kutangaza elimu bure, mwitikio wa wanafunzi umekuwa mkubwa tofauti na matarajio. Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Charles Shao amesema shule yake mpya baada ya kugawanywa, ilikumbwa na changamoto ya upungufu wa madarasa, hivyo msaada huo utasaidia kumaliza tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment