ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 15, 2016

RAPPER JOHN WOKA APATA AJALI YA KULIPUKIWA NA GESI, YUPO ICU


Rapper anayejulikana kwa kurap kama mlevi, John Woka, amepata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na rapper huyo:
Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
Mpaka hapa bado hajapata fahamu,mipango ya matibabu inaendelea. Tunasubiri kuambiwa kinachotakiwa kufanyika na mahitaji. Hospitali pale yupo kaka yake ambaye anapatikana kwa number ya Woka +255767007005 na mzee wake,kwa yoyote ambaye angependa kufika,kujua kinachoendelea au kuchangia chochote anaweza kumpigia tu moja kwa moja.

No comments: